Wednesday, April 2, 2014
SPIKA WA BUNGE LA A.MASHARIKI MASHAKANI.
Do you like this story?
Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka
kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya
uamuzi.
Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa
wabunge hao kwa niaba ya wabunge wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani
Mwinyi, amesema wabunge hao wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo
Margareth Zziwa kufuatia kukerwa na mwenendo wake.
Tayari wabunge hao wameshapeleka hoja ya
kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili
kutimiza matakwa ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili
kuanzisha hoja ya kumwondoa spika.
Je wabunge hao hawakuwa na njia nyingine
kumaliza mgogoro huo hadi kufikia hatua ya kutaka kumwondoa spika huyo.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo
umesababisha kuahirishwa kwa bunge hilo tangu jana kwa muda usiojulikana baada
ya spika huyo kuamua kuliahirisha kwa muda usiojulikana.
Hii inafuatia malumbano yalijitokeza ndani
bunge hilo ambapo mmoja wabunge alisema hoja hiyo isingeweza kujadiliwa.
BBC ilifanya juhudi za kuwasiliana na spika
huyo Margareth Zziwa kwa simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo hata hivyo
alikataa kusema chochote ambapo alishauri apigiwe afisa habari wa bunge hilo
ili atoe ufafanuzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SPIKA WA BUNGE LA A.MASHARIKI MASHAKANI.”
Post a Comment