Wednesday, April 2, 2014
MITAMBO YA ANALOJIA YAZIMWA TANZANIA.
Do you like this story?
Tanzania imeingia awamu ya pili ya
mpango wake wa mfumo wa matangazo kuhama kutoka analojia kwenda dijitali, kwa
kuzima mitambo ya analojia katika baadhi ya miji ya kati na magharibi mwa nchi
hiyo.
Miji iliyoingizwa katika mfumo huo
kuanzia jumanne wiki hii ni Singida na Tabora wakati ambapo miji mingine saba
ikiwemo Kigoma na Kagera itaingizwa kufikia mwezi Mei mwaka huu.
Mkuu wa mawasiliano wa Mamlaka ya
mawasiliano Tanzania - TCRA, Inocent Mungy ameiambia BBC mjini Singida kuwa
kufikia Novemba 30 mwaka huu watakuwa wamezima mitambo ya analojia katika miji
11 kwa awamu hii ya pili, huku akidai kuwa kazi ya kukamilisha matangazo ya
dijitali kwa nchi nzima itakuwa ndani ya muda uliowekwa.
Wakati Tanzania ikiwa mstari wa
mbele katika eneo la Afrika Mashariki , Kenya ipo kwenye mgogoro wa kisheria
kukamilisha mpango huo.
Kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa
nchi nyingi duniani zinatakiwa kuhamia matangazo ya digitali ifikapo Juni mwaka
2015.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MITAMBO YA ANALOJIA YAZIMWA TANZANIA.”
Post a Comment