Thursday, April 3, 2014
VYETI VYA KUKOSA UKIMWI VYAUZWA UGANDA.
Do you like this story?
Stakabadhi gushi za ukimwi zinauzwa
Uganda
Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika
kimebaini ushahidi wa watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya
HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizochukuliwa
kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili
kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti
hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi,
kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa
Mwandishi wa BBC wa Kampala
Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo
zilikuwa tayari kutupa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hatuna virusi vya
kusababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka
hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri
katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda Kampala
zinathibitisha kuwa unaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
Tulipomkabidhi Waziri wa Afya,
Ruhakana Rugunda, ushahidi wetu, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini
akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashtaki
wanaohusika
katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango
kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa
viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika
kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VYETI VYA KUKOSA UKIMWI VYAUZWA UGANDA.”
Post a Comment