Wednesday, June 11, 2014

SHILINGI 11 BILLIONI ZA SAFARI ZA JK ZAFYEKWA.



Bajeti y ash 50 billioni zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya safari ya rais jakaya  kikwete  katika mwaka ujao wa fedha  ni miongoni mwa mafungu ya fedha yaliyopigwa panga ili kuwezesha kupatikana kwa fedha za kugharamia miradi ya maendeleo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha majadiliano baina ya serikali na kamati ya bunge  ya bajeti zinasema  sh 11 bilioni zimepunguzwa katika fungu hilo na kubakiza sh 39 bilioni.

Hata hivyo kiasi kilichobakishwa ni ongezeko la asilimia j260  la sh 15 bilioni zilizopitishwa na bunge mwaka jana kwa ajili ya safari za rais  katika mwaka  wa fedha unaomalizika  june 30 mwaka huu.

Kwa hiyomwaka 2014/15 serikali ilimtengea rais sh 50 billioni za safri ila tumekata sh bilioni 11  ili kupeleka katika shughuli zingine za maendeleo  kwa hiyo kwa mwka ujao wa fedha safari za rais zitatengwa sh 39 bilioni.

Awali ilielezwa kuwapo kwa mvutano  mkali baina  ya serikali  na kamati ya bunge la bajeti lakini jana mchan apande hizo zilikubaliana kukata asilimia 7.5 ya fedha katika baadhi ya mafungu ya matumizi mengineyo (oc) kutoka katika wizara zote  ili kuwezesha kupatikana kwa sh 230  bilioni ambazo zinahitajika kwa  ajili ya maendeleo hata katika sekta tatu afya, miundombinu,   na kilimo.

Bado kikao kinaendelea na tangu asubuhi tumekata fedha katika fungu la matumizi mengineyo mfano chai katika ofisi   zawizara  pamoja na ununizi wa magazeti ununuzi wa magari ya kifahari  mafuta viburudisho semina na makongamano  pamoja na sagari za ndani kilieleza chanzo chetu.

Juzi naibu waziri wa fedha mwigulu nchemba alisema wizara yake inakusudia  kupitia bajeti za wizara  zote ili kuhamisha  yasiyo ya lazima ili zielezwe  katika mahitaji muhimu.

Kwa wananchi wanakula mlo mmoja kwa siku waliopo wizarani  hawawezi  kufa kwa kukosa chai hasubuhi  tutafanya hivyo ili fedha hizo zipelekwe katika shughuli za maendeleo.

Kesho(jana) katika kikao cha mashauriano tutakwenda kuweka msimamo wa pamoja katika jambo hilo wizzara zisielekeze macho  wizara ya fedha pekee nazo zinatakiwa kuwa na miakakti ya kubana matumizi yake.

Mwenyekiti wa kamti ya bunge la bajeti Andrew change alipoulizwa kuhusu hatua iliyofikiwa  katika majadiliano  alisema siburini itakaposomwa bajeti mtajua kilichoamuliwa

0 Responses to “SHILINGI 11 BILLIONI ZA SAFARI ZA JK ZAFYEKWA.”

Post a Comment

More to Read