Saturday, November 22, 2014
HALI YA USAFI JIJINI DAR KUREJESHWA KAMA ZAMANI WAKATI WA OBAMA ALIVYOKUJA
Do you like this story?
Huenda umekuwa mbali
na vyombo vya habari kufahamu kilichojiri Bungeni leo Novemba, uhali ya
mazingira ya Dar imezungumziwa, unajua ahadi aliyoitoa Waziri Aggrey Mwanri?
Wa kwanza kuuliza
swali alikuwa
Anne Kilango; “…Iwapo Serikali
iliaweza kusafisha jiji la Dar es salaam likawa safi kuzidi hata
Geneva wakati alipokuja Rais Obama pale Dar es salaam inashindwaje sasa
kumaintain hali ile ikaendelea kuweka jiji la Dar es salaam katika sura
inayopendeza na kuvutia watu wote wanaokuja Dar es salaam.“
“..Kariakoo ni kitovu
cha biashara ya jumla kwa Afrika Mashariki wanakuja wafanyabiashara wa Kenya,
wa Uganda na wafanya biashara wote wa Tanzania wanakuja Kariakoo kwa ajili ya
kuchukua biashara kwa jumla, lakini mheshimiwa mwenyekiti miundombinu ya jiji
eneo la Kariakoo sio rafiki kwa biashara, hivi Serikali haioni ni aibu kwamba
Afrika mashariki wote wanakuja kununua kwa ajili ya Kariakoo lakini imeshindwa
kutengeneza miundombini ya Kariakoo?”- Anne Kilango
Aggrey
Mwanri; “.. Nidhamu
maana yake ni kufanya jambo kama linavyotakiwa, kwa wakati unaotakiwa na mahali
linapotakiwa , kama Mheshimiwa Rais Obama alikuja hapa tukasafisha mji ukawa
msafi maana yake kulikuwa kuna discipline tulipeleka pale ndio maana
tukaonekana kama tulivyooonekana..“
Kilichofanyika
Mheshimiwa kwanza kilifanyika kitu kinachoitwa Sheria ndogo, mtu akifanya hivyo
anatozwa shilingi elfu hamsini kama ikitokea hivyo, Moshi kimefanyika kitu kama
hiki tunachozungumza Mheshimiwa Mwenyekiti na pale Moshi ndio ipo hiyo
discipline, mtu akikwangua Vocha akamaliza akatupa Barabarani wanamdaka pale
pale..“– Aggrey
Mwanri.
“..Ninachoelewa hapa
mheshimiwa mwenyekiti ni kweli kama anavyosema mheshimiwa Anne Kilango kwamba
kumekuwa kuna nini, ni kwamba sisi tunakiuka taratibu sisi wenyewe, tumemtuma
Katibu Mkuu wa Wizara ya kwetu ndugu Sabini, amekwenda mpaka Dar es Salaam,
amewachukulia hatua watendaji wote wanaohusika na mambo ya uchafu hapa,
nimesema na ninasema maneno haya kwa sababu nataka mheshimiwa msinihukumu kwa
jambo hili kama halikufanyika, sasa mimi naulizwa hapa nijibu swali na najibu
swali sasa nasema sasa sindio nimemuambia katibu mkuu wa wizara aende pale
akasimamie jambo hili kwa hiyo tumefanya hilo jambo hiyo ndio hatua ambayo
tumechukua…“– Aggrey
Mwanri.
“..Lakini mimi
nasubiria maelekezo hapa nikipewa maelekezo hapa mimi bado nitaendelea kufanya
hivyo kwa sababu mimi ndo ninayetakiwa kusimamia kazi hiyo..
Kuhusu Kariakoo ni kweli kama unavyosema Mheshimiwa ni kweli na hela zinazookotwa pale ni hela nyingi za kutosha, no hakuna mtu anaetaka kuiona Kariakoo ikaonekana kama inavyooonekana, pale palikuwaga na jitihada za kuondoa Magari pale sasa hivi at least magari yanaweza kukimbia pale, lakini I’m saying katika hii jitihada ambayo nimesema hapa, Mheshimiwa hiyo najua kitu hiki ninachozungumza hapa ni sensitive mimi napokea maelekezo haya na nataka nikuambie kwamba, tutaendelea kusimamia kuhakikisha kwamba hali hii inaondoka, pale lipo jiji, zipo na manispaa hizo ambazo nimesema hapa tutazisukuma tuhakikishe kwamba jiji la Dar es salaam linakuwa katika hali ya usafi kama wanavyosema waheshimiwa wabunge…“– Aggrey Mwanri.
John
Mnyika; “.. Mheshimiwa
Naibu Waziri hajajibu swali aliulizwa swali ni kwanini Rais Obama alikuja jiji
likawa safi kwa nini sasa hivi Serikali inashindwa kufanya jiji liwe safi? sasa
naomba kuuliza swali la nyongeza Mheshimiwa Naibu Waziri amesema hapa kwamba,
katibu mkuu wa Wizara amekuja Dar es salaam na amewachukulia hatua watendaji
wote amesema neno wote wanaohusika na usafi, mimi nina taarifa za watendaji
ambao wanakusanya fedha za wananchi lakini usafi wa mazingira haufanyiki kwenye
mitaa, anaposema kwamaba watendaji wamechukuliwa hatua atutajie ni watendaji
gani? Wakati bado watendaji wengi wanasimamia uchafu badala ya kusimamia
usafi?..“
Aggrey
Mwanri; “..Kwanza nataka
nilieweke vizuri habari ya wote ni yeye amesema hapa habari ya wote, sasa kama
si napata nafasai ya kuzungumza hapa ili ni clarify? Afadhali nilinde tuu mzee
wangu mi naomba unilinde hapa, ninachosemaa wale ambao tulibaini kwamba
wanamatatizo hatua hii mheshimiwa mwenyekiti sio hatua ndogo, kama hatua levo
ya wizara tunaweza kumuagiza mtendaji mkuu aende Dar es salaam na akapita na
akafanya ziara, ambayo najua kabisa wewe Mheshimiwa huku dispoti na yeye
Mheshimiwa Mnyika hakudispoti ni kweli wale ambao tulibaini wanafanya hivyo
tuliwachukulia hatua..“
“..Mimi Mheshimiwa
nisibishane na kiti chako niseme kwamba presha hii naiona naipokea hii
changamoto niyakwangu mimi kwa sababu ndio msimamizi wa jambo hili, mimi
nitakwenda kuchukua hatua zote zinazotakiwa na mi nitahamia hapo Dar es Salaam,
nikihamia Dar es salaam itakuwa ni vurugu tuu..”– Aggrey Mwanri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HALI YA USAFI JIJINI DAR KUREJESHWA KAMA ZAMANI WAKATI WA OBAMA ALIVYOKUJA ”
Post a Comment