Friday, November 14, 2014
MBEYA CITY FC WANA KIBARUA KIZITO KUFUTA 'SHUBIRI' HII.
Do you like this story?
Mechi nyingine iliyoweka rekodi mpaka
kufikia raundi ya saba ni ile ya Mgambo JKT dhidi ya Mbeya City fc iliyopigwa
uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga oktoba 3 mwaka huu.
Awali mechi hii ilipangwa kuchezwa
Oktoba 2 mwaka huu, lakini kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Tanga,
uliahirishwa kufuatia uwanja kujaa maji.
Mbeya City fc waliokuwa na hamu ya
kushinda baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo, bao 1-0 dhidi ya Azam fc na
mabao 2-0 na Mtibwa Sugar uwanja wa Sokoine walijikuta wakifungwa mabao 2-1 na
Mgambo.
Wakiendelea kujiuliza nini kimetokea,
wakajikuta wakifungwa tena 1-0 na Stand United, Oktoba 8 mwaka huu uwanja wa
CCM Kambarage Shinyanga.
Rekodi iliyowekwa na Mbeya City msimu
huu ni kufungwa mechi nne mfululizo na kushika mkia katika msimamo wa ligi kuu
ikijikusanyia pointi tano tu.
Pia ni timu pekee iliyofunga mabao
mawili tu, tena moja la penati ya Deogratius Julius kwenye mechi dhidi ya
Coastal Union iliyochezwa septemba 27 mwaka huu uwanja wa Sokoine Mbeya.
Deus Kaseke aliifungia bao la pili
msimu huu katika kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Mgambo JKT.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MBEYA CITY FC WANA KIBARUA KIZITO KUFUTA 'SHUBIRI' HII.”
Post a Comment