Friday, November 14, 2014

.MIILI YA WATOTO WADOGO YAOKOTWA BAHARI YA HINDI JIJINI DAR




Taarifa ambayo imetolewa kwenye kipindi cha XXL na kwenye akaunti ya Facebook ya Clouds FM inasema kuwa kuna miili ya watoto wadogo imeokotwa kwenye pwani ya bahari ya Hindi Msasani kwenye maeneo ya karibu na Baraka Plaza.

Miili ya watoto hawa ambao wanaonekana kufanana, wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 10 ambapo shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Polisi walifika na kuichukua miili hiyo wakati wa mchana.

Watu walioiona walisogea mpaka Mbalamwezi Beach na kuomba simu ipigwe Polisi kwa hiyo tukio hili halikutokea Mbalamwezi beach wala miili hii haikuokotwa kwenye eneo hili.

0 Responses to “.MIILI YA WATOTO WADOGO YAOKOTWA BAHARI YA HINDI JIJINI DAR ”

Post a Comment

More to Read