Tuesday, June 23, 2015

MADEREVA WATAKAOGOMA SAFARI HII SASA WATAFUKUZWA KAZI




MADEREVA wa mabasi watakaofanya mgomo bila kufuata utaratibu, wakati kukiwa na hatua za kutafuta ufumbuzi wa masuala yao watafukuzwa kazi, imeelezwa.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Nchini (Taboa), Enea Mrutu ambapo alisema, bado kuna mjadala unaoendelea hivyo si sahihi kwa madereva kugoma.

Alisema kama kuna dereva yeyote anayetaka kugoma, anapaswa mgomo huo akaufanyie kwa tajiri yake na si vituoni na kusababisha watu wengine kushindwa kuendelea na shughuli zao.

Mrutu alisema, hivi karibuni wakati Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta akiwasilisha bajeti yake, madereva hao waliitisha kikao bila kutoa taarifa kwa wamiliki, jambo lililosababisha wao kutoshiriki kikao hicho.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Nchini (Chamamata), Clement Masanja alisema mgomo wao utakuwa palepale endapo kikao cha serikali na wamiliki hakitatoa majibu ya matatizo yao.

Mambo hayo ni pamoja na utaratibu wa nauli ya kwenda na kurudi majumbani baada ya kazi, matibabu, usafiri, likizo pamoja na bima.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema, hawezi kuingilia mgogoro huo lakini kama watakwenda kumuona kama madereva walivyoahidi ataangalia namna ya kuwashauri.

0 Responses to “MADEREVA WATAKAOGOMA SAFARI HII SASA WATAFUKUZWA KAZI ”

Post a Comment

More to Read