Wednesday, June 3, 2015

SHUGHULI ZA UOKOAJI ZAENDELEA CHINA.


Wafanyakazi wa uokoaji wakiwa karibu na eneo ilipozama meli


Waziri wa Usafirishaji wa China amesema wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanawapata watu walionusurika miongoni mwa mamia ya waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa meli katika mto Yangtze kutokana na hali mbaya ya hewa.

Maelfu ya waokoaji walifanya kazi usiku kucha katika meli hiyo iliyopinduka ijulikanayo kama "Nyota ya Mashariki" katika jimbo la Hubei.

Watu saba wamethibitika kufa na wengine 14 wamekutwa hai katika meli hiyo iliyokuwa na watu 456.
Ndugu waliojawa na hasira wanalalamikia kukosekana kwa taarifa za uokoaji.

Watu walionusurika ni pamoja na nahodha wa meli na mhandisi mkuu, wote wawili wakiwa katika mahabusu za polisi.

Nahodha amesema meli hiyo ilikumbwa na kimbunga na kuzamishwa chini ya mto katika dakika chache.BBC

0 Responses to “SHUGHULI ZA UOKOAJI ZAENDELEA CHINA.”

Post a Comment

More to Read