Wednesday, June 3, 2015
TFF YATOA ONYO KALI MBA, YANGA.
Do you like this story?
Na
Bertha Lumala, Dar es Salaam
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limezionya kiana klabu kongwe za soka nchini, Simba na
Yanga baada ya kuweka wazi kwamba halitaidhinisha usajili wa wachezaji wapya wa
klabu ambazo zimeshindwa kuwalipa nyota waliowahi kuzitumikia.
Katibu
mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, aliyasema hayo katika mahojiano na kipindi cha
Sports Bar cha Clouds TV, ikiwa ni muda mfupi baada ya kurejea kutoka Zurich,
Uswisi alikokuwa amehudhuria mkutano mkuu wa uchaguzi wa Rais wa Shirikisho la
Soka la Kimataifa (FIFA).
"Itafikia
kipindi Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF haitapitisha usajili wa
wachezaji wapya wa klabui ambazo bado hazijawalipa wachezaji ambao waliwahi
kuzitumikia.
"Maana
unakwendaje kuona mke wa pili wakati mke wako wa kwanza umeshindwa kumtimizia
mahitaji kiasi cha kufikia hatua ya kuzunguka mitaani kusaka mahitaji
muhimu," alisema Mwesigwa.
Ingawa
hakuweka wazi klabu ambazo alikuwa anazilenga, kauli ya Mwesigwa ni kama onyo
kwa klabu kongwe nchini, Simba na Yanga ambazo zimekuwa na tabia ya kuwaacha
wachezaji pasipo kuwatimizia mahitaji yao.
Februari
4 mwaka huu FIFA iliipa Simba siku 30 kuhakikisha inamlipa aliyekuwa beki wake
wa kati Donald Mosoti dola za Marekani 13,800 (Sh. milioni 27.6) kutokana na
kusitisha mkataba wa Mkenya huyo.
Katika
barua yake kwa TFF iliyokuwa na anuani ya FAX +4143/222 77 55, FIFA iliagiza Simba
kumlipa Mosoti ndani ya muda huo dola 13,800 na penalti ya asilimia tano (5%)
ambayo ni dola za Marekani 600 kutokana na kumharibia mipango yake kisoka
kuanzia Desemba 12, 2013 walipomtimua hadi siku ambayo malipo yatafanyika.
Mbali
na kuvunja mikataba ya Waganda Danny Sserunkuma na Simon Sserrunkuma mara tu
baada ya kumalizika msimu uliopita, Simba pia inadaiwa dola la Marekani 17 (Sh.
milioni 34) na mfungaji bora wa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL)
msimu wa 2013/14, Amissi Tambwe kutokana na klabu hiyo ya Msimbazi kuvunja
mkataba na Mrundi huyo Desemba 14 mwaka jana.
Yanga
pia ilishawahi kuagizwa na FIFA kumlipa beki wa kushoto John Njoroge Sh.
million moja za Kenya (Sh. milioni 10 za Tanzania) baada ya klabu hiyo ya Jangwani
kuvunja makataba wake kienyeji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TFF YATOA ONYO KALI MBA, YANGA.”
Post a Comment