Monday, June 22, 2015
ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA JULAI 4 JIJINI DSM
Do you like this story?
Viongozi wa
chama cha mapinduzi kata ya Jangwani Ilala jijini Dsm, wametakiwa kuhamasisha
wananchi kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la kudumu la
wapiga kura linalotarajia kuanza julai 4 jijini Dsm.
Akizungumza katika mkutano maalum na viongozi hao Mbunge wa ilala Mussa Azzan Zungu, amesema Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu na umejaa changamoto mbalimbali ikiwemo ushindani mkali ndani ya CCM pamoja na vyama vya upinzani.
Amesema licha ya chama cha mapinduzi kujivunia wingi wa Wanachama, lakini wasipojitokeza kujiandikisha katika daftali la wapiga kura wanaweza kusababisha chama hicho kupoteza nafasi mbalimbali za uongozi.
Wakati Huo huo Kikundi cha Vijana cha wajasiliamali cha Ilala - Mchikichini kimewataka vijana kubadili mtazamo kuhusua ajira na kujishughulisha katika kazi za ujasiliana zitakazoleta tija na kuwainua kiuchumi.
Vijana hao wametoa wito huo baada ya kukabidhiwa mashine za kufyatuali matofalipamoja na mifuko ya SARUJI 50 kwa ajili ya kuimarisha biashara yao utengenezaji wa matofari na kuuza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA JULAI 4 JIJINI DSM ”
Post a Comment