Monday, June 22, 2015

UMMOJA WA MADEREVA NCHINI WATISHIA KUGOMA KWA MUDA USIOJULIKANA.


Umoja wa madereva nchini umetangaza nia yake ya kugoma kwa muda usiojulikana kama mufaka hautafikiwa kati yao na wamiliki pamoja na serikali kuhusu kutatuliwa kwa madai yao makuu ambayo ni pamoja na kuwa na ajira zinazoeleweka.

Tangazo hilo linakuja kufuatia vikao walivyoketi kwa tarehe za 18 na 19 mwezi june mwaka huu ambapo hata hivyo havikuzaa matunda baada ya wamiliki wa mabasi nchini kushindwa kuhudhulia jambo ambalo linatajwa kuwa ni dharau kwa madereva, ambapo kupitia kwa msemaji wa umoja huo wa madereva nchini Bw.Rashid Saleh anasema hawaoni sababu ya kuendelea kulumbana na waajili wasiojali maslahi yao na kwamba sasa huenda wakaamua kupumzika kwa muda usiojulikana mpaka pale matatizo yao yote yatakapo tatuliwa kikamilifu na si kwa ahadi tena.
 
Kwa upande wao madereva waliofurika katika ukumbi wa kimara resot kusikia tamko hilo wanasema wamekwisha kuchoshwa na ahadi zisizo tekelezeka nakwamba endapo kikao cha june 23 mwaka huu kitashindwa kuzaa matunda wako tayari kuachana na kazi hiyo kwani hakuna chochote wanachokipata kwa muda mrefu sasa.
 
Katika hatua nyingine mjumbe wa kamati kuu ya umoja wa madereva Tanzania Bw. Moris Jumanne amewataka madereva hao licha ya kudai haki zao kwa nguvu lakini pia lazima wahakikishe wanakuwa mstali wa mbele katika kutii na kuheshimu kanuni za barabarani kwani bila kufanya hivyo ajali zitazidi kuongezeka kila siku.
 
Endapo watashindwa kufikia muafaka katika mkutano wake na wamiliki pamoja na serikali kuhusu mustakabali wa maslahi katika kazi, huu utakuwa mgomo watatu ndani ya kipindi kifupi ambapo kwa muda wote huo wananchi ndio wamekuwa waathirika wakuu

0 Responses to “ UMMOJA WA MADEREVA NCHINI WATISHIA KUGOMA KWA MUDA USIOJULIKANA.”

Post a Comment

More to Read