Saturday, December 12, 2015

‏ RATIBA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA




Yanga imepangwa kuanza na mabingwa wa Mauritian, Cercle de Joachim katika draw ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali iliyopangwa usiku wa kuamkia leo mjini Dakar, Senegal

Katika draw hiyo, Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania Bara, wamepangwa kuanzia ugenini, mchezo utakaopigwa kati ya Februari 12 na 14 mwakani, kabla ya kurudiana Bongo kati ya Februari kati ya Februari 26 na 28, 2016.

Takwimu zinaonyesha, Joachim haina rekodi nzuri, imekuwa mabingwa nchini mwao mara mbili tu; 2014 na 2015. Uwanja wao wa Stade George V, unachukua watu 6,200 tu.

Mshindi kati yao, anakutana na mshindi kati ya Mbanane Swallows ya Swaziland na APR ya Rwanda.

Mafunzo, wawakilishi wa Tanzania Visiwani, wamepangwa kuanzia nyumbani kwa kuwakaribisha wakongwe wa michuano hii, AS Vita ya DR Congo . Ndio kaimu bingwa wa kombe hili kwa sasa, baada ya kulikosa mwaka huu mbele ya ES Setif ya Algeria.

Azam katika draw ya Kombe la Shirikisho, wamepangwa kuanzia hatua ya pili (16 Bora) wakisubiri mshindi kati ya Bidvets Wits ya Afrika Kusini na bingwa wa FA wa Visiwa vya Seychelles. JKU kwa upande wa Visiwani, wapo hatua ya awali wakianzia nyumbani kuwavaa Gaborone ya Botswana.

0 Responses to “‏ RATIBA YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA”

Post a Comment

More to Read