Friday, December 11, 2015

UKAWA WASHINDA KITI CHA MEYA MBEYA MJINI.


Madiwani wateule wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakila kiapo(Picha na David Nyembe wa Fahari News)
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Dr Samweli Lazaro akionyesha Karatasi la Kupigia Kura kwa Madiwani.

Diwani akipiga Kura

Diwani wa Kata ya Forest Hery Mwangambako akipiga Kura

Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dr Samweli Lazaro akimpongeza Meya wa Jiji Bw David Mwashilindi mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Meya wa Jiji la Mbeya Mch David Mwashilindi( kushoto) akiwa na Naibu  Meya Mch David Ngogo mara baada ya kutangazwa kuwa washindi(Picha na David Nyembe wa Fahari News)






CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata ushindi mkubwa jana katika uchaguzi wa kugombea nafasi ya Meya na Naibu Meya watakaoongoza halmashauri ya jiji la Mbeya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wagombea walioteuliwa na Chama hicho ni, Mch David Ponela Mwashilindi kutoka kata ya Nzovwe kugombea nafasi ya Mstahiki Meya wa jiji hilo  na  Mch David Nelson Ngogo  kutoka kata ya Nsalaga aliyegombea kiti cha Naibu Meya.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Mkapa na kusimamiwa na Katibu tawala wa wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela,alimtangaza mshindi wa Umeya kuwa ni Mwashilindi aliyepata kura 34 akimshinda mgombea wa nafasi hiyo kutoka CCM,Kefas Mwasote Changani aliyeambulia kura 14.

Kwa upande wa nafasi ya Naibu Mbeya mshindi wa kura nyingi aliyetangazwa ni Mch Ngogo(Chadema) aliyeipata kura 34 dhidi ya mgombea wa CCM katika kinyang’anyiro hicho,Modest Pantaleo Shiyo aliyeambulia kura 14 na hivyo kukifanya chama cha Chadema kuongoza halmashauri ya jiji hilo.

Mara baada ya kutangaza matokeo hayo yaliyowashirikisha madiwani wa Chadema 34 dhidi ya wale wa CCM 14,msimamizi wa uchaguzi huo,Mbeyela alisema kuwa vyama vyote vilivyoshiriki kwenye mchakato huo sasa umekwisha na wanachotakiwa kukifanya madiwani wote ni kuchapa kazi kwa nguvu ili kusukuma kwa kasi maendeleo ya jiji hilo.

Akizugumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Naibu Meya,Ngogo amesema kuwa atahakikisha kuwa anaheshimu haki na uhuru wa kila diwani katika kushauri na kutoa maoni bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa kuwa kazi kubwa iliyo mbele yao  ni kuwatumikia wananchi wote.

Mstahiki Meya wa jiji hilo kutoka Chadema,Mwashilindi akiwashukuru madiwani wote kwa kura nyingi alizopigiwa,amesema kuwa atahakikisha kuwa anashirikiana na madiwani wote na kuhakikisha kuwa kata zote za jiji hilo zinapiga hatua kubwa na huo ndio mtazamo wake.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Dk Samwel  Lazaro alisema kuwa atahakikisha watendaji wa halmashauri hiyo wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote pale wanapohitaji ufafanuzi wa kitaalamu ili kila jambo wanalotaka kulifahamu wapate  kwa wakati.

Mwisho.

0 Responses to “UKAWA WASHINDA KITI CHA MEYA MBEYA MJINI.”

Post a Comment

More to Read