Friday, December 11, 2015
ATEMWA YANGA, ASAINI MIAKA MIWILI KOREA
Do you like this story?
Hans Mloli, Dar es Salaam
KIUNGO wa pembeni, Mbrazili, Andrey Coutinho, aliyesitishiwa mkataba na Klabu ya Yanga, mwanzoni mwa wiki hii, tayari amepata dili la kusaini miaka miwili kuitumikia Kwampong inayoshiriki Ligi Kuu ya Korea.
KIUNGO wa pembeni, Mbrazili, Andrey Coutinho, aliyesitishiwa mkataba na Klabu ya Yanga, mwanzoni mwa wiki hii, tayari amepata dili la kusaini miaka miwili kuitumikia Kwampong inayoshiriki Ligi Kuu ya Korea.
Inajulikana kuwa chanzo kikubwa cha kuondoka
kwa mchezaji huyo klabuni hapo ni kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha
kwanza cha timu hiyo kilichopo chini ya Kocha Mholanzi, Hans van Der Pluijm
lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, amefafanua kilichokuwa nyuma ya
pazia.
Tiboroha ameliambia Championi Ijumaa kuwa
Coutinho ameuzwa akiwa kama mchezaji huru ambavyo ni tofauti na watu
walivyokuwa wakifikiria lakini pia amekanusha taarifa za kwamba wao ndiyo
waliomtema mchezaji huyo na badala yake ni kwamba Coutinho alitaka kuondoka
mwenyewe.
“Coutinho amepata dili la kucheza miaka
miwili huko Korea kwenye timu ya Kwampong. Coutinho ameondoka akiwa kama
mchezaji huru baada ya kumalizana naye katika mkataba wake uliobaki, kuhusu
tulilipana au ilikuwaje, hiyo inabaki kuwa siri yetu lakini ndivyo ilivyokuwa.
“Unajua ningependa watu waelewe kwamba
Coutinho si kwamba tulimuondoa, ni kwamba aliomba kuondoka yeye mwenyewe na
ishu ilikuwa ni kutopata nafasi, kwa hiyo tukamalizana naye na sasa yupo
Korea,” alisema Tiboroha.
Kuondoka kwa Coutinho kikosini hapo, kumetoa nafasi ya Yanga kuvuta mchezaji mpya wa kimataifa, Mniger, Issofou Boubacar kumfanyia majaribio na kama akifuzu, basi watamsajili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ATEMWA YANGA, ASAINI MIAKA MIWILI KOREA”
Post a Comment