Friday, December 11, 2015
PROFESA LIPUMBA, LISSU WAPINGA UTEUZI WA MUHONGO NA MWAKYEMBE.
Do you like this story?
Saa chache
baada ya rais Magufuli kutangaza baraza lake la Mawaziri ambalo limekuwa baraza
dogo kama alivyoahidi, aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na
mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu wamekosoa uteuzi wa Profesa
Sospeter Muhongo na Dk. Harison Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe
alikuwa waziri wa Uchukuzi katika serikali ya awamu ya nne na hivi sasa
ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria. Profesa Muhongo ambaye alijiuzulu
kwa kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne, amerudishwa katika wizara
ya Nishati na Madini.
Profesa Lipumba
amekosoa uteuzi wa profesa Muhongo kwa madai kuwa uteuzi wake umelitia doa
baraza hilo.
“Kwa kitendo
kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana na uteuzi huu. Maana yake
ni kuwa katika kashfa ile Profesa Muhongo hakuwa na hatia,” Profesa Lipumba
aliliambia gazeti la Mwananchi.
Profesa Lipumba
aliongeza kuwa wananchi watapata ugumu kumuelewa Rais kutokana na ahadi zake
kuwa atapambana na rushwa na ufisadi.
Naye Tundu
Lissu aliliambia gazeti hilo kuwa uteuzi wa Dk. Harison Mwakyembe hakuwa sahihi
kwa kuwa ndiye aliyekuwa waziri wa Uchukuzi na punde baada ya rais Magufuli
kuingia ikulu, Mamlaka ya Bandari ikabainika kukumbwa na kashfa ya upotevu wa
makontena.
“Juzi Rais
Magufuli aliufumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa,
miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk. Harrison Mwakyembe,
eti leo amemrudhisha kundini?” Lissu ananukuliwa.
Lissu aliongeza
kuwa Muhongo pia hakufaa kuwa miongoni mwa mawaziri kwa kuwa alifukuzwa na
Bunge kutokana na sakata la Escrow.
Hata hivyo,
Profesa Lipumba alimpongeza rais kwa kutekeleza ahadi yake ya kuunda baraza
dogo kwa lengo la kubana matumizi.
Mpekuzi blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ PROFESA LIPUMBA, LISSU WAPINGA UTEUZI WA MUHONGO NA MWAKYEMBE. ”
Post a Comment