Tuesday, December 8, 2015
SCHWEINSTEIGER ATUPWA JELA YA FA
Do you like this story?
Kiungo wa Manchester United, Mjerumani
Bastian Schweinsteiger 31, anakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na
chama cha soka England (FA) kutokana na kitendo chake cha kumpiga kiwiko usoni
mlinzi wa Westham United, Winston Reid katika mchezo uliomalizika kwa sare ya
bila kufungana Jumamosi iliyopita.
Schweinsteiger ana hadi Alhamis hii, saa sita
mchana kukubali/kukataa kosa hilo baada ya FA kumuadhibu Jumatatu hii. Refarii
Marc Clatternburg aliwaita wachezaji wote wawili na kuongea nao, huku asichukue
hatua nyingine yeyote kutokana na kutoona tukio hilo.
Chama cha waamuzi kupitia video wamebaini
kosa hilo la Bastian Schweinsteiger lililotokea kabla ya mapumziko na sasa
mchezaji huyo anaweza kufungiwa hadi mechi tatu zinazosimamiwa na chama cha
soka England, FA.
Habari hizi sio nzuri kwa Manchester United
ambayo inakabiriwa na majeruhi ya viungo wake wengine Morgan Schneiderlin na
Ander Herrera huku Bastian Schweinsteiger akiwa miongoni mwa watu muhimu katika
kikosi hicho hivi sasa.
Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal
akizungumzia tukio hilo anasema hakuona chochote na hivyo hana la kufanya zaidi
ya kuwaachia wenye mamlaka kutimiza sheria. Kocha wa Westham Bilic amesema kuwa
Bastian alistahili kadi nyekundu lakini akasisitiza hawezi mlaumu mwamuzi kwani
hakua katika kona nzuri ya kuona tukio hilo.
Beki wa kati wa Westham aliyefanyiwa tukio
hilo Winston Reid alisema kuwa Bastian mwenyewe anajua alichomfanyia na hivyo
kutokana na mwamuzi kutoona tukio hilo, lakini alistahili kutolewa nje kwa kadi
nyekundu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SCHWEINSTEIGER ATUPWA JELA YA FA”
Post a Comment