Tuesday, December 8, 2015
MAHAKAMA KUMKAMATA MBUNGE LWAKATARE
Do you like this story?
Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana
ilitishia kumkamata Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare baada ya kutokuwapo mahakamani hapo.
Kauli ya Hakimu Thomas Simba
imetolewa baada ya Mdhamini wa mshtakiwa, Paschal Mwita kudai mahakamani
hapo kuwa mshtakiwa huyo hakuwapo mahakamani na kwamba amesafiri kwenye
shughuli zake za ubunge.
Wakili Mwandamizi wa serikali,
Pamela Shinyambala alidai kuwa barua ya ruhusa ya mshtakiwa huyo ambaye hivi
sasa ni Mbunge wa Bukoba Mjini, ameiona leo (jana) na kwamba upelelezi
haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine.
Hata hivyo, Hakimu Simba alionya
kuwa ubunge wake (Lwakatare) usiwe sababu ya kuahirisha kesi hiyo na alipanga
kuisikiliza tena Desemba 21 mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Lwakatare na
Joseph Ludovick wanadaiwa kuwa Desemba 28, 2013 katika eneo la King’ongo,
Wilaya ya Kinondoni, kwa pamoja walikula njama za kujaribu kumdhuru aliyekuwa
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky kwa njia ya sumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAHAKAMA KUMKAMATA MBUNGE LWAKATARE”
Post a Comment