Tuesday, December 8, 2015
WATIWA MBARONI KWA KUPIGA PICHA VIFAA VYA JWTZNA KUVISAMBAZA MITANDAONI
Do you like this story?
JESHI la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema limeanza kuchukua hatua kali kwa watu
waliohusika na upigaji wa picha wa vifaa vya kijeshi na kusambaza kwenye
mitandao ya kijamii, ambapo hadi sasa tayari watu wanne wapo chini ya ulinzi.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa
JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga alisema kumekuwa na tabia ya kusambaa kwa taarifa,
zisizotakiwa kusambazwa na kusababisha usumbufu kwa taasisi za Serikali na hasa
Jeshi.
“Desemba 3, mwaka huu
saa 1:15 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, lilitokea
tukio lisilo la kawaida lililotendwa na wafanyakazi wa shirika la kupokea
mizigo la Swiss Port wakishirikiana na wenzao wa Shirika la Ndege la KLM kwa
kupiga picha vifaa vya kijeshi na kusambaza katika mitandao ya kijamii,” alisema Kanali
Lubinga.
Alisema mizigo hiyo
ni mali ya JWTZ na kuagizwa kwake, hakujaanza hivi karibuni kama baadhi ya watu
katika mitandao ya kijamii wanavyoeleza, bali ni matokeo ya hatua
zilizochukiliwa na JWTZ kupitia Wizara ya Ulinzi miaka sita iliyopita katika
mpango wake wa kujenga uwezo wa JWTZ.
“Tunasikitika kwa
tukio hili la watu kujichukulia maamuzi ya kupiga picha kitu ambacho
hakikuwahusu na pia kusambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii na
kupelekea kujitokeza kwa maoni ya kupotosha jamii,” aliongeza
Mkurugenzi huyo katika JWTZ.
Alisema tabia za
kupotosha jamii, zimetokea mara kwa mara na hivyo kuvunja mshikamano uliopo
kati ya Serikali na wananchi wake, jambo ambalo jeshi hilo halitalifumbia
macho.
Alisema ni kwa msingi
huo, wameanza kuwasaka wahusika wote, ambapo tayari watu wanne wapo chini ya
ulinzi na watachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine, kutokana na
upigaji wa picha hizo na usambazaji wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATIWA MBARONI KWA KUPIGA PICHA VIFAA VYA JWTZNA KUVISAMBAZA MITANDAONI”
Post a Comment