Monday, January 11, 2016
CUF YAPINGA MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.
Do you like this story?
Chama
cha Wananchi (CUF) kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani
Zanzibar.
Chama
hicho kupitia taarifa kwa wanahabari kimesema hakuna “hoja wala msingi wa
kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa”.
Taarifa
ya chama hicho ambayo imesomwa na mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25
Oktoba mwaka jana Maalim Seif pia inaonekana kupendekeza mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ang’atuke.
Chama
hicho kimemtuhumu Rais wa visiwani Mohamed Ali Shein wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) kwa kukwamisha mashauriano ya kutafuta suluhu ili ZEC itangaze marudio ya
uchaguzi tarehe 28 Februari 2016.
CCM
imeonekana kuunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi visiwani na majuzi viongozi wa
chama hicho waliwataka wafuasi wake visiwani kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tangazo
hilo lilishutumiwa vikali na viongozi wa CUF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ CUF YAPINGA MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.”
Post a Comment