Thursday, January 14, 2016
SERIKALI YATUMIA BILION 459 KWENYE MIKOPO YA WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016
Do you like this story?
Serikali
imetumia bilioni 459 kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha
mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi 122,486 wamenufaika.
Hayo yamesemwa
na Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa
Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo
Jijini Dar es salaam.
“Walionufaika
na mikopo katika kipindi cha 2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea katika
Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi na haya ni matokeo ya utendaji mzuri
wa Serikali ya awamu ya tano “alisisitiza
Ngole
Akizungumzia
utolewaji wa mikopo Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa
jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na jumla bilioni 341 zilitolewa .
Pia Ngole alibainisha
kuwa Serikali imeongeza idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia vipaumbele
vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.
Ngole
amebainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya
Serikali ya awamu ya tano inayosema Hapa Kazi tu.
Aliongeza kuwa
Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya
tano itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa kuzingatia sheria Kanuni. na
Taratibu za utoaji mikopo.
Bodi ya Mikopo
ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa
sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi julai, 2005 ambapo Katika mwaka
wa Masomo 2005/2006 idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ilikuwa 42,749 ambapo
jumla ya bilioni 56.1 zilitolewa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATUMIA BILION 459 KWENYE MIKOPO YA WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016 ”
Post a Comment