Thursday, January 14, 2016
ZOEZI LA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LAPAMBA MOTO MKOANI MBEYA
Do you like this story?
Na jamiimojablogu,Mbeya
Zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu na wageni
wanaofanya kazi bila kibali limeendelea kufanikiwa mkoani Mbeya ambapo jumla ya
wageni 20 wamekamatwa mkoani humo kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la
kuingia nchini kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini
kwakwe Afisa uhamiaji Mkoa wa mbeya Ndugu Asumsyo Achacha amesema hatua hiyo
imefanyika ikiwa ni kutekeleza majukumu yao ya kila siku sanjali na kutekeleza
agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Charles Kitwanga alilotoa hivi karibuni.
Aidha amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa
sheria mpya ya kuratibu ajira za wageni ,Sherii Na.1 ya mwaka 2015 ambayo
inawataka wageni wote walioajiliwa hapa nchini kuwa na vibali vya kazi na hati
za ukaazi nchini.
Afisa uhamiaji huyo amewataja raia hao
waliokamatwa katika msako huo ni pamoja wakenya watatu (3)wamalawi 14 pamoja na
wakongo watatu (3).
Aidha amesema kuwa mwaka 2015 jumla ya
wahamiaji haramu 478 kutoka mataifa mbalimbali walikamatwa na kuchukuliwa hatua
mbalimbali ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini.
Amesema mbali na changamoto zilizojitokeza
ikiwemo upungufu wa vitendea kazi ,fedha pamoja na rasilimali bado
shughuli za uhamiaji mkoani humo ziliendelea kufanyika kama kawaida na kwa
ufanisi mkubwa.
Pia Afisa Uhamiaji huyo amebainisha kuwa zoezi
hilo ni endelevu hivyo ofisi yake itahakikisha kila mtu aliyevunja sheria
anakamatwa hivyo ametoa wito kwa waajiri kuacha tabia ya kuwapa ajira
wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kazi na ukaazi kwani msako huo utaendelea
katika viwanda ,migodi mashuleni na mahotelini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ZOEZI LA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LAPAMBA MOTO MKOANI MBEYA”
Post a Comment