Tuesday, January 12, 2016
TAARIFA YA UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI YA KUDUMU ZA BUNGE
Do you like this story?
TAARIFA
KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.
Katibu wa Bunge
anatoa taarifa kwa umma kwamba:
(a) Kwa mujibu
wa Kanuni ya 116 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013, Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amepewa mamlaka ya kuteua Wajumbe wa Kamati za
Kudumu za Bunge kwa namna ambayo itawezesha kila Mbunge kuwekwa kwenye Kamati
mojawapo. Katika kufanya uteuzi huo, Spika huzingatia vigezo mbalimbali
vilivyoainishwa katika Kanuni ya 116 (5);
(b)
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Mhe. Job Yustino Ndugai (MB),
ametekeleza mamlaka yake ya uteuzi kwa mujibu wa Kanuni tajwa hapo juu, kwa
kuwateua kwanza Wabunge Kumi na Tano (15) kuwa Wajumbe wa Kamati ya Kanuni za
Bunge.
Kamati
hiyo imeundwa na kutangazwa kabla ya Kamati zingine ili ifanye marekebisho ya
Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge kuhusu majukumu ya Kamati zingine
za Bunge kwa kuyashabihisha na majukumu ya Serikali kwa kuzingatia Muundo wa
Baraza la Mawaziri lililopo sasa.
Lengo
kuu ni kuleta urahisi, ufanisi na tija kwa Bunge katika kuisimamia na kuishauri
Serikali;
(c)
Kwa msingi huo, Kamati ya Kanuni za Kudumu za Bunge, ambayo Spika ndiye
Mwenyekiti wake na Naibu Spika ni Makamu Mwenyekiti, Kiongozi wa Upinzani na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni Wajumbe kwa nyadhifa zao itakutana katika
Ofisi ya Bunge, Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 15 Januari, 2016 saa tano
kamili asubuhi katika Ukumbi wa Spika. Wajumbe wengine ni: –
(i)
Mhe. Makame Kassim Makame, MB. – Jimbo la Mwera;
(ii)
Mhe. Tundu Antipas Mughwai Lissu, MB. – Jimbo la Singida Mashariki;
(iii)
Mhe. Jasson Samson Rweikiza, MB. – Jimbo la Bukoba Vijijini;
(iv)
Mhe. Ally Saleh Ally, MB. – Jimbo la Malindi;
(v)
Mhe. Magdalena Hamis Sakaya, MB. – Jimbo la Kaliua;
(vi)
Mhe. Salome Wycliff Makamba, MB. – Viti Maalum;
(vii)
Mhe. Dkt. Jasmine Tiisekwa Bunga, MB. – Viti Maalum;
(viii)
Mhe. Zainab Athman Katimba, MB. – Viti Maalum;
(ix)
Mhe. Balozi Adadi Mohamed Rajab, MB. – Jimbo la Muheza;
(x)Mhe.
Dkt. Charles John Tizeba, MB. – Jimbo la Buchosa; na
(xi)
Mhe. Kangi Alphaxard Lugola, MB. – Jimbo la Mwibara.
(d)
Spika atakamilisha uteuzi wa Wajumbe katika Kamati zingine za Bunge kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Bunge tarehe 26 Januari, 2016, Mjini Dodoma ili
kutoa fursa kwa Kamati zote kuchagua Viongozi wake na kuandaa Mpango Kazi kwa
mwaka 2016/17; na
(e)
Wabunge wote wanatangaziwa kuwa wawe wamefika Dodoma tarehe 20 Januari, 2016
tayari kwa kuanza kwa Kamati za Bunge na Mkutano wa Bunge, isipokuwa Kamati ya
Wabunge (Caucus) wote wa Chama cha Mapinduzi wanatakiwa kuwa Mjini Dodoma
tarehe 17 Januari, 2016 kwa Mkutano wao.
Imetolewa
na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM.
11 Januari, 2016.
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
S. L. P. 9133,
DAR ES SALAAM.
11 Januari, 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAARIFA YA UTEUZI WA WABUNGE KWENYE KAMATI YA KUDUMU ZA BUNGE”
Post a Comment