Monday, November 28, 2016

NECTA YAIFUNGIA SHULE KUFANYA MTIHANI WA TAIFA KWA MIAKA 3 MFULULIZO




Baraza la mtihani la Taifa NECTA imeifungia shule ya msingi ya Little Flower Englishi Medium inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Musoma kutofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa kutumia kituo, hicho baada ya kubainika kufanya udanganyifu mkubwa wa majibu ya matokeo ya darasa la saba katika mtihani ambao umefanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Akitangaza uamuzi huo wa NECTA katika kikao cha kuchagua wanafunzi wa kujinga na kidato cha kwanza mwaka kesho, afisa elimu wa mkoa wa Mara Bw Hamis Lisu, amesema mbali na kituo hicho kufungiwa kufanya mtihani huo katika kipindi cha mwaka 2017 hadi 2019, pia matokeo yote ya wanafunzi 37 waliofanya mtihani huo mwaka huu katika kituo hicho wilayani Serengeti pia yamefutwa.

Naye katibu tawala mkoa wa Mara Bw Adoh Mapunda, akizungumza katika kikao hicho cha uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza, ameonya tabia ya baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari kujihusisha na vitendo vya udanganyifu, na kwamba amesema serikali itachukua hatua kali katika kukomesha vitendo hivyo.


0 Responses to “NECTA YAIFUNGIA SHULE KUFANYA MTIHANI WA TAIFA KWA MIAKA 3 MFULULIZO”

Post a Comment

More to Read