Wednesday, December 21, 2016

WENYE VVU WALILIA KUKOSA DAWA




Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wilayani Temeke wamesema wanakabiliwa na changamoto ya Ukosefu wa dawa za kukabiliana na magonjwa nyemelezi kutoka katika hospitali za wilaya hiyo lakini pia wamedai kuwapo madhara kutokana na kubadilishiwa dawa za kupumbaza virusi vya UKIMWI-ARV.
Akizungumza wakati wakipatiwa fedha kiasi cha shilingi million 64 kutokana manispaa ya Temeke kwa ajili ya mitaji ya biashara ya ujasiliamali kwa vikundi 51 vya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi manispaa ya Temeke,M/kiti wa mtandao wa watu wanaishi na VVU Said Kambangwa anaeleza.

Katibu tawala wa manispaa ya Temeke Hashim Komba amewataka watu wanaishi na VVU wasikate tamaa kwa kuwa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi itahakikisha inawasaidia kwa hali na mali ili kuimarisha afya zao lakini pia kuendesha biashara na ujasilimali ili kuongeza kipato kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

Aidha Vikundi hivyo vya watu wanaoishi na VVU wamependekeza kuundwa Mfuko wa Taifa wa Ukimwi- Aids Trust Fund kuanzia ngazi ya kata,wilaya hadi mkoa ambapo vikundi hivyo katika wilaya ya temeke vina jumla ya wanachama wanawake 1260 na wanaume 480.

0 Responses to “ WENYE VVU WALILIA KUKOSA DAWA”

Post a Comment

More to Read