Friday, December 23, 2016

BWANA HARUSI ALIYEINGIA MITINI ARUDI NA KUFUNGA NDOA.MBEYA


Maharusi wakiwa na nyuso za Furaha mara kufunga Pingu maisha katika kanisa la KKKT Isanga jijini Mbeya


Bi harusi Given Mgaya akimvisha pete bwana harusi Samwel ishara ya uaminfu kwake wakti wakifunga ndoa katika kanisa la KKKT Isanga Mbeya.

Waandishi wapiga kambi kufatilia kitakacho jiri katika kanisa la KKKT Isanga










HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.

Ndoa hiyo imefungwa leo  majira ya saa tisa Desemba 23  katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.

Kabla ya  maharusi hao kula kiapo cha ndoa,Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.





Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.

Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.

Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.
Mara baada ya kufungisha ndoa hiyo nje ya kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari bwana harusi Mwakalobo alisema kuwa anawaomba radhi ndugu jamaa na marafiki na kwamba kilicho tokea ni mapito.

“ndugu zangu nawadhibitishia kuwa alipangelalo mungu binadamu hawezi kulitengua ni kwe;li tuliopnga tarehe ile lakini sisi ni wanadamu mungu alipanga huu ulikuwa ni upepo ulipita na niwaombe radhi ndugu jamaa kwa hili liliotokea” alisema Mwakalobo
Aidha katika hatua nyingine bibi harusi aligoma kuzungumzia suala hilo huku kwa kile alichokileza lile suala lililotokea kila kitu anamwachia Mungu.







0 Responses to “BWANA HARUSI ALIYEINGIA MITINI ARUDI NA KUFUNGA NDOA.MBEYA”

Post a Comment

More to Read