Saturday, December 24, 2016
PENZI LA BIBI WA MIAKA 60 LAUA KIJANA WA MIAKA 23
Do you like this story?
KIJANA
mwenye umri wa 23 na mpenzi wake, bibi mwenye umri wa miaka 60 , wakazi wa
kijiji cha Tentula, Kata ya Ikozi wilayani Sumbawanga, wanashikiliwa na polisi
wakihutumiwa kumshambulia na kumuua kikatili jirani yao aitwae Desder Justino
(23) kwa kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Inaelezwa
kuwa, Justino pia alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bibi huyo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo na kueleza
kuwa mauaji hayo yalitokea Desemba 21 mwaka huu saa nne asubuhi katika nyumba
ya mwanamke huyo iliyopo kijijini Tentula.
Taarifa
kutoka kijijini humo zinadai kuwa, mwanamke huyo licha ya umri wake kuwa
mkubwa, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana hao wawili wa rika moja.
Kamanda
Kyando hakuwa tayari kutaja majina ya wapenzi hao ambao ni watuhumiwa wa mauaji
kwa sababu za uchunguzi.
Lakini
alisema mwanaume ana umri wa miaka 23 huku mpenzi wake ana umri wa miaka 60.
Akielezea zaidi, Kamanda Kyando alisema siku ya tukio Justino alikwenda
nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi
na kumkuta kijana mwingine (mtuhumiwa), na hapo ndipo ugomvi ukaibuka baina ya
vijana hao.Alisema Justino alijeruwa kichwani.
“Wawili
hao yaani wapenzi hao (mwanamke na mwanaume) walimshambulia Justino (Desder)
kwa kumpiga kichwani na kitu chenye ncha kali na kumjeruhi vibaya na alikufa
akiwa anatibiwa hospitalini,”
alisema Kamanda Kyando na kuongeza kuwa, watuhumiwa hao wanashikiliwa na
watafikishwa mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ PENZI LA BIBI WA MIAKA 60 LAUA KIJANA WA MIAKA 23”
Post a Comment