Sunday, January 15, 2017
KUKIONA CHA MOTO WALE WANAOPOTOSHA KUWA WANATIBU UKIMWI
Do you like this story?
Tume
ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) kwa kushirikiana na vyombo vya dola
inatarajia kuanza operasheni maalumu hivi karibuni ya kuwasaka baadhi ya
viongozi wa madhehebu ya dini na waganga wa tiba za asili wanaowapotosha
wagonjwa wa ukimwi wanaotumia madawa ya kufubaza virusi vya ugonjwa huo kwa
kuwashawishi waache kutumia madawa hayo badala yake waishi kwa imani ya uponyaji
wa njia ya miujiza.
Akizungumza
na waandishi wa habari,Mwanasheria wa TACAIDS,Elizaberth Mzelu, amesema
sheria namba 27 inayohusiana na masuala ya kinga dhidi ya ugonjwa wa
ukimwi iliyotungwa mwaka 2008 inamzuia mtu yoyote kujitangaza kuwa anatibu ukimwi
au anamkinga mtu asipate virusi vya ukimwi.
Kwa
upande wake,Dkt.Subilaga Kaganda Mtaalamu wa afya ya jamii wa TACAIDS amesema
serikali ina mkakati mkubwa wa kumaliza tatizo la maambukizi ukimwi ifikapo
mwaka 2030 na ameeeleza kuwa mkakati huo kwa sasa unatekelezwa katika hatua
mbalimbali.
Naye,Mratibu
wa mkoa wa Kagera wa ICAP Dkt.Omary Msumi ameiomba serikali iendelee kutoa
elimu juu umuhimu wa matumizi wa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi,Charles
Mwafimbo afisa ustawi wa jamii mkoani Kagera aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa
warsha ya kujadili mpango kazi wa taifa wa kinga ya ukimwi wa kuanzia mwaka
2016-2018 kwa niaba ya Katibu Tawala Kagera Kamishina Diwani Athumani ameagiza
kamati za kupambana na ukimwi kuanzia ngazi za vijiji zifufuliwe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ KUKIONA CHA MOTO WALE WANAOPOTOSHA KUWA WANATIBU UKIMWI”
Post a Comment