Monday, February 6, 2017
LIQUID TELECOM YA KAMILISHA UNUNUZI WA KAMPUNI YA KUTOA HUDUMA ZA INTANET TANZANIA .
Do you like this story?
Meneja Mauzo wa Kampuni Bi Blandina Mahawanga akizungumza juu ya mikakati ya Biashara nchini Tanzania |
Picha ya Pamoja |
Katika
kukuza soko la mawasiliano nchini kammpuni tanzu ya Econet Global Pan African
Telecom group Liquid Telecom imekamilisha ununuzi wa kampuni ya kutoa huduma ya
internet inayoongoza nchini Tanzania inayojulikana kama RAHA
kampuni
ya Liquid Telecom ni mdau mpya wa kampuni
hiyo kwa kumiliki hisa nyingi na wamejikita katika kuimarisha sehemu ya Raha katika soko la Tanzania kwa kuwekeza
Zaidi kwenye mtandao na huduma.
Raha
itakuwa kama sehemu ya mtandao mkubwa wa mkonga mkuu wa Liquid Telecom, ikitoa mtandao
mmoja kwa biashara nyingi tofauti. Mtandao huu umeanzia Cape Town ukapita Dar
es salaam na kuelekea Nairobi; ambao unaumbali wa kilomita 40,000
naukiunganisha nchi 12.
Pia
hii itaboresha ushindi wa tuzo kwa Liquid
Telecom kwenye East Africa Fiber Ring (mkonga unaozunguka Africa Mashariki) ambayo inaunganisha
Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania moja kwa moja kwenye mkonga wa kimataifa.
Hili ni eneo la kwanza lenye fibre ring ya ziada yenye chaguzi ya njia Zaidi ya moja ili kuhakikisha kwamba wateja hawaathiriki
na kukatika kwa mkonga na kupotea kwa mtandao.
Nic
Rudnick ni AfisaMtendaji Mkuu wa Liquid Telecom ambaye wanayofuraha sana kuikaribisha
Raha katika Liquid Telecom group na Tanzania inakua kwa kasi kubwa mno na soko
la Afrika linalo badirika mara kwa mara Na kwakupitia ununuzi huu tutaweza kumudu
kwa kiasi kikubwa mahitaji ya kupata mtandao kwa nchi nzima
Pia
alieleza kuwa Liquid Telecom inapanga kuongeza
kwa kiasi kikubwa idadi ya vituo vya Wi-Fi ya bure kwa hapa Tanzania, ilikuweza
kuziba pengo liliopo katika ulimwengu wa kidijitali kwa kuiwezesha
idadi kubwa ya watu kupa taintaneti na kusema Raha imeshaanzisha zaidi ya vituo 150 vya
Wi-Fi ya bure katika miji yote mikubwa ya Tanzania. Vituo hivyo vinatumika na zaidi
ya watumiaji 150,000 wakipekee
Aashiq
Shariff ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Raha “Kwa kuwezeshwana Liquid Telecom,
Raha inaweza kupata njia mpya zakuonge za muunganiko kwa hapa Tanzania ikiwemo na
maeneo mengine. Pia tutafaidika na ujuzi na utaalamu wa makampuni ya Liquid
Telecom Group hivyo kutusaidia kufikia dira yetu ya Tanzania iliyounganishwa zaidi”,
alisema
Ikumbukwe
Liquid Telecom ni kampuni inayoongoza na kujitegemea katika kutoa huduma za
data, sauti na IP katika Afrika mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya kusini.
Inatoa huduma za mkonga mkuu, satellite na huduma za simu za kimataifa kwa watoa
huduma wa simu za mkononi wa hapa Afrika, watoa huduma za mtandao, taasisi za kifedha
na mabiashara yenye ukubwa tofauti.
Pia
Liquid Telecom imejenga mkonga mmoja mkubwa Afrika wa mtandao ambao kwa sasa unaumbali
wa kilomita 40,000 ikijumuisha mtandao wa Neotel, ukivuka mipaka na kufunika uchumi
unaokua kwa kasi Afrika ambapo hakuna mtandao wa kudumu uliokuwepo hapo awali.
Ikifanya kazi katika chapa tofauti, Liquid Telecom Group inavituo vya kazi
Botswana, DRC, Kenya, Lesotho, Mauritius, Rwanda, Afrika Kusini, Tanzania,
Uganda, Uingereza,
Zambia na Zimbabwe.
Kwa
miaka 5 iliyopita, kampuni hii imepewa jina la kampuni bora ya mauzo ya jumla
.........................................
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “LIQUID TELECOM YA KAMILISHA UNUNUZI WA KAMPUNI YA KUTOA HUDUMA ZA INTANET TANZANIA .”
Post a Comment