Tuesday, January 31, 2017
MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya
kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja
na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.
Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti
shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele
cha upandaji miti kimkoa katika eneo la
chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya.
Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na
kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa
mazingira katika maeneo yot.
"Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile
iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli
za kibInadam"Alisema Makala.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akipanda mti katika kilele cha Upandaji kimkoa katika chanzo cha Maji Hanzya Kata ya Itagano. |
Meya wa Jiji la Mbeya David Mwashilindi akipanda Mti katika kilele cha upandaji Miti katika safu ya Mlima Mbeya. |
Askari
wa JKT Itende Mbeya pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na
Usafi wa Mazingira jijini Mbeya (UWSA) na baadhi ya watumishi
halmashauri ya jiji la Mbeya wakiendelea na zoezi la upandaji miti
katika Safu ya Mlima Mbeya katika Chanzo cha Maji Hanzya Itagano Jijini
Mbeya
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw William Ntinika akipanda Mti katika kilele cha upandaji Miti katika safu ya Mlima Mbeya. |
Wanafunzi wa shule ya Msingi Itagano wakiwa katika zoezi la kupanda Miti |
Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda
miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo
vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya
kila siku.
"Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua
milioni 1 kwa mwaka katika kila
halmashauri mkoani humo ambapo mwezi
juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja
kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema .
Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango
wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana
kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara
baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI”
Post a Comment