Tuesday, January 24, 2017
MAENDELEO BANK WASOGEZA FURSA KWA WAFANYABIASHARA KARIAKOO
Do you like this story?
Askofu
Mkuu wa Diosisi ya Mashariki na Pwani wa kanisa la KKKT Dkt Alex Malasusa
Amewaasa wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kujifunza njia sahihi ya
kuhifadhi akiba kwenye mabenki ili kuepukana matatizo yanayoweza kuwakumba kama
kuibiwa fedha hususani katika kipindi hiki kigumu cha upatikanaji wa fedha. Pia
aliwaomba kuitumia Maendeleo Bank kwa ajili ya biashara zao kupitia huduma za
mikopo.
Askofu Malasusa
ameyasema hayo tarehe 23.01.2017 alipokuwa akizungumza na Fahari news katika uzinduzi wa tawi
jipya la benki ya (Maendeleo Bank) lililozinduliwa kariakoo
Jijini Dar es Salaam
Meneja
wa tawi hilo jipya Bi Nuru Shedrack alisema uzinduzi wa tawi hilo la Kariakoo
linatoa fursa kwa wafanyabiashara kwa kusogezewa huduma ya kibenki karibu na
sehemu zao za kazi ili kuepuka usmbufu na hatari ya kutembea na fedha jambo
ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao.
Aidha
Bi Nuru alifafanua kuwa licha ya Maendeleo Bank kuwa chini ya Kanisa la KKKT
ila Benki hiyo inalenga kutoa huduma kwa watu wote bila kujali itikadi za
kidini, chama wala kabila.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Maendeleo Bank Bw. Ibrahim Mwangalaba alisema Bank ya Maendeleo
itaendelea kuboresha utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na Kusogeza Karibu zaidi
Huduma zake kwa wateja.
Hili
ni tatu la pili kuzinduliwa na Benki hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam, ambapo
tawi la kwanza lilizinduliwa Novemba mwaka 2016 eneo la Mwenge Jijini hapa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAENDELEO BANK WASOGEZA FURSA KWA WAFANYABIASHARA KARIAKOO ”
Post a Comment