Thursday, March 13, 2014
BREAKING NEWS: SAMIA SULUHU HASSAN ACHAGULIWA RASMI KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA.
Do you like this story?
Hatimaye
bunge maalum la katiba limemchagua Mh. Samia Suluhu Hassan kuwa makamu
mwenyekiti wa bunge hilo, katika uchaguzi huo uliofanyika muda huu bungeni
Dodoma
Akitangaza
matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo amesema Mh. Samia amepata kura 390 sawa
na asilimia 74.6 huku mgombea mwenzake Mh. Amina Abdalah Amour akipata kura
126, ambapo kura 7 zimeharibika
Kwa
matokeo hayo Mh Samia amekuwa makamu mwenyekiti mteule wa bunge maalum la
katiba
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa, Mh. Samia amesema anamshukuru mpinzani wake kwa kumpa
wakati mgumu ikiwemo kigezo cha kukubalika ndani ya bunge, pamoja na wanawake
wote waliopo ndani ya bunge hilo kwa kumpa ushindi huo
Awali
Mh. Amina yeye amekubaliana na matokeo hayo, na kuongeza kuwa kwa kuwa aliyeshinda
ni mwanamke, basi ushindi huo ni wa wanawake wote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BREAKING NEWS: SAMIA SULUHU HASSAN ACHAGULIWA RASMI KUWA MAKAMU MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA.”
Post a Comment