Thursday, March 13, 2014
SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU VITAMBULISHO KWA WAANDISHI BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Do you like this story?
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akizungumza na wabahabari (hawapo pichani) kuhusu utoaji wa Vitambulisho vya Waandishi wa Habari kwenye shughuli za Bunge Maalum la Katiba. |
SERIKALI
imetoa ufafanuzi juu ya vitambulisho vya waandishi wa habari ( Press card)
wakati wa Bunge Maalum la katiba na kusema kuwa ndicho kigezo pekee
kitakachowezesha waandishi wa habari kutimiza majukumu yao vyema katika
kipindi chote cha bunge hilo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari
Maelezo, Assah Mwambene wakati akitoa tamko la Serikali kufuatia taarifa
potofu zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.
Mwambene
alibainisha kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo si mgeni
kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kwamba unaweza kukipata
ndani ya saa 24 ikiwa tu mwandishi anakidhi vigezo.
Alisema
vitambulisho vinatolewa tu kwa mwandishi mwenye taaluma ya uandishi wa habari
kutoka chuo kinachotambulika naSerikali kwa kuzingatia sheria na kanuani
zilizowekwa.
Alisisitiza
kuwa utaratibu wa kutoa vitambulisho kwa waandishi habari upo
na ni wa kisheria hivyo ni lazima ufuatwe.
Pia
amesema kuwa ni vyema kila mwandishi akafuata taratibu zote za kupata
kitambulisho kinachotolewa na MAELEZO kwa kuwa bila kitambulisho hicho hataweza
kufanya kazi katika kazi rasmi kama vile Bunge maalum la katiba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU VITAMBULISHO KWA WAANDISHI BUNGE MAALUM LA KATIBA.”
Post a Comment