Monday, March 31, 2014

JELA MIEZI SITA KWA WIZI WA JENEZA.




 Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu imemhukumu Bahati Lukas (25) kifungo cha nje miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa jeneza.

Mwanamke huyo mkazi wa kijiji cha Nyaumata, Kata ya Somanda mjini Bariadi alihukumiwa kifungo hicho baada ya kukiri.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Samwel Kilabuka alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 19 mwaka huu eneo la Somanda.

Alidai mshtakiwa alifika maeneo yanapochongwa na kuuzwa majeneza hayo na aliulizia bei ya jeneza ili auziwe.
Kilabuka alidai mshtakiwa baada ya kuambiwa bei ya jeneza alisimama, huku muuzaji akiendelea na shughuli nyingine. Inadaiwa hatua hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kubeba jeneza hilo kichwani na kutoweka nalo.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikiri kutenda kosa, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya, Robart Oguda alimhukumu kifungo cha nje miezi sita.
Hakimu Oguda alisema mahakama ilibaini mshtakiwa alikuwa na matatizo ya akili, ikiwamo pia ugumu wa hali ya maisha yake

0 Responses to “JELA MIEZI SITA KWA WIZI WA JENEZA.”

Post a Comment

More to Read