Friday, March 14, 2014

KIFICHO AWAONYA WALE WASIOVAA MAVAZI RASMI.




Dakika 10 baada ya Bunge maalumu la katiba kupitisha kanuni zake, mwenyekiti wa muda wa bunge hilo pandu ameir kificho aliwataka wajumbe kuanza kuvaa nguo za heshima na kuonya wakikiuka jambo hilo kanuni zitawaumbua.

Akizungumza bungeni  juzi baada ya kusomwa kwa azimio la kuridhia kanuni hizo kificho aliwataka wjumbe kuachana na mavazi waliyokuwa wakivaa wakati wa semina za bunge hilo.

Mavazi yanapaswa kuvaliwa na wajumbe waakati wa vikao rasmi ni suti ya safari yenye mikono mifupi au mirefu ikiwa na rangi nyeusi au blue na wanawake ni suti ya rangi nyeusi au bluu  wakati wa semina baadhi ya wajumbe walikuwa wakivaa mavazi ya kawaida kama mashati yasiyokuwa ya kuchomekea na suruali za jeans viatu vya wazi na mashati ya vitenge.

Baadhi ya wanawake walikuwa wakivaa nguo fupi na za kubana.

Katika ufafanuzi wake kificho amesema: waheshimiwa wajumbe sasa tumepata kanuni hivyo ni lazima mjitazame vizuri mavazi yenu hakikisheni kuwa hamvai mavazi ambayo ni kinyume na kanuni mlizozitunga wenyewe alikumbusha kificho

0 Responses to “KIFICHO AWAONYA WALE WASIOVAA MAVAZI RASMI.”

Post a Comment

More to Read