Friday, March 14, 2014
SITTA: KURA Y A SIRI.
Do you like this story?
Mwenyekiti mteule wa Bunge
maalumu la katiba Samuel sitta
amezungumzia uwezekano wa kutumia kura ya sira katika kuamua
idara nyeti katika rasimu ya
katiba.
Sitta aliyechaguliwa juzi
kuhika wadhifa huo alisema atashirikiana na kamati ya uongozi itakyoundwa
ya wenyeviti wa kamati 15 za
bunge hilo na kamati ya ushirikiano
kupata jawabu la suala hilo.
Akizingumza katika
mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, sitta alisema: unajua kuna
baadhi ya vifungu na ibara za rasimu ya katiba ni vizuri vipigiwe
kura ya wazi na vingine ambavyo ni nyeti
zaidi vipigiwe kura ya siri”
Amesema si vizuri vifungu
vyote vipigiwe kura sawa yaani si
lazima zote ziwe za siri au ziwe za wazi.
Alitoa mfano wa ibara
inayosema kutakuwa na mahakama kuu ya Tanzania na kusema: “Hatuwezi kushindana
katika suala la kuwapo kwa mahakama ni ni wazi kuwa jambo hilo mnaweza kupiga kura ya wazi nasema hivyo kwa sababu
kativa yoyote lazima ionyesha mihimili yote ambayo bunge, serikali na Mahakama.
Sitta ambaye pia ni waziri
wa ushirikiano wa Afrika Mashariki alishinda kiti hicho katika uchaguzi
uliofanyika juzi kwa kura 487 kati ya 563(sawa sawa na asilimia 85)
Mbunge huyo wa urambo mashriki ambaye kaulimbiu yake ni kasi na viwango alisema vifungu na
ibara za rasimu ya katiba vinavyoweka misingi ya kativa ni vizuri vikapigiwa
kura ya siri.
Unajua tuna viongozi wa
dini na halitakuwa jambo la busara kama
tukizijua hisia zao. Kama wewe uko karivu na imamu au askofu halafu anapiga
kura ya wazi ya kutaka serikali tatu wkati wewe muunini unataka serikali mbili
ni wazi kuwa jambo hilo linaweza kuleta hisia tofauti na kuwanyima watu haki na
uhuru wa kuamua alisema sitta.
Alitoa mfano wa sura ya
sita ya rasimu ya katiba inayozungumzia
serikali na muundo wa madaraka
katika jamhuri ya mungano na
kufafanua kuwa katika sura hiyo atapendekeza
ipigiwe kura ya siri.
Kuhusu suala hilo la
muundo wa serikali alisema kikubwa ni
wajumbe kujenga hoja hatuwezi kwenda na msimamo isiyobadilika kwa sababu
tunataka maridhiano . nitatenda haki na
nitatoa muda mrefu zaidi kwa wajumbe kujadili sura ya kwanza nay a sita ambazo
zina uzito mkubwa kuliko sura nyingine
ambazo ni za maelezo tu. Mano suala la haki za binadamu ambazo wote
tunakubaliana nazo.
Amesema wakati wa kujadili
moundo huo wa serikali ndani ya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ukifika
ataishauri kamati ya uongozi kutenga
muda wa ziada katika suala hilo na
mengine yenye utata.
Mwenyekiti huyo alisema
suala la upigaji kura linatakiwa kuamuliwa kwa busara na atatumia hekima zake
na za wajumbe wa bunge hilo kutatua mgogoro wa kura ya siri au ya wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SITTA: KURA Y A SIRI.”
Post a Comment