Thursday, March 20, 2014

KINGUNGE AKERWA NA SERIKALI 3.




MWANASIASA wa siku nyingi muumini wa siasa ya ujamaa kingunge ngombale mwiru, amesema tume ya mabadiliko  ya katiba ya jaji warioba  imeangaliza zaidi kero  za muungano katika kudai  serikali tatu hali ambyao inavunja muungano.

Akizungumza katika mahojiano maalumu alisema tume ilipaswa kuangalia changamoto  zilizopo ili zirekebishwe na kuimarisha muugnano lakini  si kushauri kuvunja  kwa kuunda serikali tatu.


Tume ingeenda na kazi ya kujenga na sasa inabomoa kwani wamekuwa wakitazama zaidi kasoro baada ya kuona kuna kero kwenye muungano wangeleta marekebisho na kufanya kazi ya kuleta mapendekezo alisema.

Amesema kuruhusu serikali tatu tutakuwa na nchi ya ajabu hilo limefanyika wapi duniani? Serikali tatu kwenye nchi moja  akaohoji kingunge.

Amesema marekani wana serikali zaidi ya 50 na wamekuwa wazalendo  kwenye nchi yao na hakuna wa kuwagusa hata china na indiaa wako vivyo hivyo.

Amesema suala la kuwa na katiba mpya kuna haja ya kutafakari  na kuona cha kufanya na kuhakikisha inapatikana kativa bora zaidi kuliko  iliyopo sasa na bila hivyo hakuna sababu ya kupata katiba mpya.

Pamoja na hayo amesema tume ya marekebisho ya katiba haikuheshimu  wananchi na mapendekezo  katika sura ya kwzna juu ya kuungano wa Tanzania kwani mapendekezo  yao ni kuundwa kwa shirikisho  .

Amesema rasimu hiyo haizungumzii  jamhuri ya muungano  wa Tanzania iliyopo  leo na uhalali wake baada ya kuundwa kwa shirikisho  la nchi mbili.

Aidha amesema ili kupata shirikisho wanaounda shirikisho wanaanza na ushirika.

Tatizo la wenzetu wa tume wanafanya kazi ya kuuliza wananchi  na wameangalia zaidi kero kwenye suala la muungano lakini kero ziko katika aina zote za serikali  hata serikali za shirikisho  zina kero zake amesema.

0 Responses to “KINGUNGE AKERWA NA SERIKALI 3.”

Post a Comment

More to Read