Thursday, March 20, 2014

MICROSOFT YAJA NA JIBU LA TATIZO LA WIZI MITANDAONI.




Kampuni ya Microsoft inayojishughulisha na utengenezaji wa kompyuta pamoja na proframu imebuni mbinu mpya  ya kukabiliana na wizi wa mitandaoni ambao umezisababishia hasara benki, kampuni na watu binafsi  katika maeneo mengi duniani.

Mkakati huo umekuja wakati benki nyingi  nchini zikiathiriwa  na wizi huo kupitia mashinde za kutolea fedsha maarufu kama ATM  pamoja na miamala inayofanyka kupita mifumo ya mawasiliano  ya kompyuta.

Takwimu zinaonyesha katika kipindi cha oktoba 2012  hadi februari 2013  tanzania inakadiriwa kuwa n ash 700 milioni ziliibiwa  katika benki  kwa nyakati tofauti.

Kutokana na halihiyo Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu aliziagiza taasisi za fedha  kuchukua hatua ili kukabiliana na hali hiyo.

Taarifa kwa vyambo vya habari iliyotolewa na mkurugenzi  mkuu wa kampuni ya Microsoft , David Finn  imeeleza kuwa wamebuni kompyuta  mpya pamoja na program ambazo zinaziba mianya ya wizi.

Imeweka wazi kuwa uuzaji holela wa program za kompyuta duniani umekuwa chanzo cha wezi hao kutumia ujanja huo katika kufahamu taarifa za siri zilizohifadhiwa  kwenye kompyuta  za taasisi zn hata watu binafsi  zilizounganishwa kwenye mtandao.

Utafiti ulitolewa mwka huu na kampuni ya kimtaifa ya teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta  ikishirikiana na chuo kikuu cha Singapore unayonyesha wizi  wa kwenye mtandao unaogharimu kampuni zaidi ya dola za kimarekani  billion 315 kwa mwaka sawa na sh 504 trilioni.

0 Responses to “MICROSOFT YAJA NA JIBU LA TATIZO LA WIZI MITANDAONI.”

Post a Comment

More to Read