Sunday, March 30, 2014

KUTOKAMILIKA KWA MIRADI MINGI KWA WAKATI JIJINI MBEYA WADAU WATOA USHAURI.


Soko jipya la Mwanjelwa jijini Mbeya ambalo ujenzi wake umekuwa wa kusuasua


Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dkt.Samweli Razaro, akifafanua kero mbalimbali za wafanyabiashara jijini Mbeya


Wafanyabiashara mbalimbali wa jiji la mbeya wakiwa katika ukumbi wa Mkapa uliopo maeneo ya Soko matola.


HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, imeshauriwa kupunguza posho za madiwani wakati wa vikao vya baraza kutokana na kushindwa kupitisha miradi ya maendeleo inayotekelezeka kwa wakati.

Ushauri huo, umetolewa jijini Mbeya  na wafanyabiashara wa Jiji la Mbeya kwenye  mkutano na uongozi wa halmashauri uliokuwa ukijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ya ongezeko kodi.
Wamesema,  miradi mingi ya maendeleo inayopitishwa na baraza hilo imeshindwa kutekelezeka kwa wakati hivyo ni vema  uongozi wa halmashauri ukawapunguzia kiwango cha posho wahusika ili kiendane  na kipimo cha uwajibikaji.
.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dkt.Samweli Razaro, ambaye licha ya kuahidi kulichukua suala hilo na kulifikisha kwenye mamlaka husika lakini alitumia nafasi hiyo kuwafafanulia wafanyabiashara sababu zilizosababisha kushindwa kukamilika kwa wakati  ujenzi wa soko la Mwanjelwa.

Amesema, awali ujenzi huo ulikuwa chini ya mkandarasi kutoka Kampuni ya Tanzania Bulding Works Limitted ya Jijini Dar es Salaam ambaye alikiuka makubaliano ya mkataba hivyo   halmashauri kuvunja na kuingia mkataba mpya na mkandarasi  kutoka Kampuni ya Nandhra  Engineering & Construction Company.

Hata hivyo,Dkt, Razaro  alisema kuwa  mkandarasi huyo mpya anatarajia kutumia shilingi bilioni 5.0 katika kukamilisha ujenzi wa soko hilo na kukabidhi kwa uongozi wa halmashauri ifikapo mwezi Desember mwaka huu.
Mwisho.

0 Responses to “KUTOKAMILIKA KWA MIRADI MINGI KWA WAKATI JIJINI MBEYA WADAU WATOA USHAURI.”

Post a Comment

More to Read