Sunday, March 23, 2014
MTALII KUTOKA UJERUMANI AKWAMA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO.
Do you like this story?
Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kama Bi. Jeanne Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa mbili na nusu asubui wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala kwenda juu.
Bi.
Jeanne na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic Tours
tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia ya Rongai - Kibo –Marangu safari ambayo
ingewachukua siku tano.
Hadi
sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni
Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na kuelekea kilele
cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum
inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.
Shirika
la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na
jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao wanaelekea eneo la tukio pamoja na
helikopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa
itakavyotulia ambapo hivi sasa kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.
Umma
utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri
zitakavyopatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTALII KUTOKA UJERUMANI AKWAMA KWENYE KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO.”
Post a Comment