Thursday, March 20, 2014
NEWS ALERT: MENEJA WA BAA YA ROSE HILL ILIYOPO TABATA SEGEREA, DEODATUS LUSINDE AFARIKI DUNIA LEO WAKATI AKISHANGILIA GOLI LA YANGA .
Do you like this story?
Wachezaji wa Yanga wakishangilia
bao lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili kulia), wakati wa mchezo wa
Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ilipopambana na Azam FC kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. bao
la Didier Kavumbagu (wa pili kulia) lililopelekea mauti ya Deodatus
Lusinde.
SHABIKI wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya
Lusinde, mkazi wa Kipunguni A, amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla
wakati akishangilia bao la Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika
ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu amepoteza maisha akiwa chumba cha
matibabu mara baada ya kuwekewa mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha
shabiki huyo zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa
uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya.
Bwana Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill
iliyopo Segerea jijini Dar. Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni
askari magereza.
Marehemu amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi
ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo
uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mungu ailaze roho ya
mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN!
Chanzo GPL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NEWS ALERT: MENEJA WA BAA YA ROSE HILL ILIYOPO TABATA SEGEREA, DEODATUS LUSINDE AFARIKI DUNIA LEO WAKATI AKISHANGILIA GOLI LA YANGA .”
Post a Comment