Thursday, March 13, 2014
RAIS WA GAMBIA AFUTA KIINGEREZA KUWA LUGHA YA TAIFA NCHINI KWAKE.
Do you like this story?
Rais wa Gambia Yahya Jammeh |
RAIS wa
Gambia Yahya Jammeh (ﻳﺤﻴﻰ ﺟﺎﻣﻊ) amesema anataka kutekeleza mabadiliko
ya sheria yatakayopelekea lugha rasmi ya nchi hiyo kubadilishwa
kutoka Kiingereza hadi lugha asili. “Hatuamini tena kuwa ukitaka
kuwa Serikalini
lazima
uzungumze Kiingereza. Inafaa tuzungumze lugha yetu,” Rais Yahya
Jammeh alisema hayo wakati wa kuapishwa kwa Jaji Mkuumpya nchini
humo. Tangazo hilo lilitolewa miezi michache baada ya nchi hiyo
kutangaza inajiondoa kutoka Jumuiya ya Madola,
inayojumuisha mataifa 54 yaliyokuwa chini ya ukoloni
wa Uingereza. Gambia ilisema “haitakuwa tena mwanachama wa
taasisi ya ukoloni mamboleo”. Uingereza ilionya hivi majuzi
kuhusu pingamizi la rais huyo dhidiya Uingereza, ambaye mwaka jana
alishutumu Uingereza na Amerika kwa kuandaa majaribio
ya mapinguzi ya Serikali nchini humo.
Rais wa
Gambia mwaka jana aliiambia dunia kupitia Mkutano mkuu wa Umoja
wa Mataifa kwamba tishio kubwa linalotishia ustaarabu na utu
wa mwanadamu ni kuwepo kwa kampeni na uhamasishaji wa
Ushoga na usagaji.
"Wale
wote wanaokuza
ushoga ni kama wanataka kukomesha kuwepo
kwa binadamu",aliuambia mkutano wa viongozi wa Dunia mjini
New York kwa mujibu wa Gazeti la Huffington Post."Hili ni janga
na sisi waislamu na waafrika tutapigana kumaliza
tabia hii".Aliongeza kwa kusema,"Ulawiti katika
namna yoyote ile ni uovu na ni kama kupambana na Mwenyezi
Mungu.
Hata kama
italazimishwa kwa nguvu fulani kuwa ni haki kwa
mwanadamu". "Gambia ni nchi ya waumini. Dhambi
na matendo ya zinaa yapolakini Ushoga si wa kuvumiliwa katika nchi
ya Gambia", aliongeza Rais Yahya Jammeh. Awali aliwaambia
mashoga waondoke nchini Gambia au watakatwa vichwa.
Mahusiano
ya jinsia moja nchini Gambia ni haramu.Mwaka 2009 Jammeh aliwaambia
maafisa wa jeshi waliopandishwa vyeo kwamba, hatutahamasisha
usagaji na ushoga katika jeshi, Ni mwiko katika
majeshiyetu,"Ntamfukuza mwanajeshi yoyote atakaye tuhumiwa kuwa
Shoga au Msagaji katika Gambia. Sisi hatuna haja ya Mashoga
katika majeshi yetu", alisema Rais huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS WA GAMBIA AFUTA KIINGEREZA KUWA LUGHA YA TAIFA NCHINI KWAKE.”
Post a Comment