Sunday, March 23, 2014
SASA SHABIKI ATAKAYEINGIA NA KUKU UWANJA WA TAIFA KUGUNGWA JELA.
Do you like this story?
SHABIKI
yeyote atakayeingia uwanjani na mnyama yeyote iwe kuku au njiwa atakumbana na
rungu la sheria ya kufungwa jela siku 90 au faini ya Sh. 100,000.
Katika
siku za hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa na kawaida ya kuingia
uwanjani na ndege wakiwemo kuku au njiwa na kuwashikilia muda wote wa mchezo
kitendo kinachozua usumbufu kwa mnyama.
Akizungumza
na Mwanaspoti, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ustawi wa Wanyama Tanzania (Taweso),
Dk. Thomas Kahema alisema, mtu yeyote anayeingia na wanyama uwanjani anapaswa
kuhakikisha anampatia huduma muhimu mnyama vinginevyo anashtakiwa kwa mujibu wa
sheria ya wanyama ya mwaka 2008.
“Sheria
ipo wazi, tukimkuta mtu wa aina hiyo anapigwa faini ya Sh. 100,000 au anaenda
jela kwa muda wa miezi mitatu, hairuhusiwi kubughudhi wanyama, pale uwanjani
kuna kelele na huwa wanawanyima uhuru wanyama,” alisema Kahema.
Naye
Mkuu wa Vikosi vya Mbwa na Farasi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Mrakibu
Mwandamizi Dk. Eugene Emmanuel aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Huo ni
ukatili wa wanyama na hairuhusiwi kuingia na mnyama yeyote uwanjani bila sababu
ya msingi, nazungumza na askari wangu kuwapa agizo kumkamata yeyote
atakayeingia na ndege uwanjani bila sababu ya msingi.”
Hata
hivyo shabiki wa Yanga, Ally Ramadhani, ambaye amekuwa akionekana na kuku mara
nyingi Uwanja wa Taifa amewahi kusema kwamba huwa anaingia na
kuku huyo uwanjani kwa imani ya timu yake kupata mabao.
Aliingia
na kuku mmoja Yanga ilipocheza na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika na
timu hiyo ikashinda bao 1-0.
SOURCE:
MWANASPOTI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SASA SHABIKI ATAKAYEINGIA NA KUKU UWANJA WA TAIFA KUGUNGWA JELA.”
Post a Comment