Thursday, April 24, 2014
JIJI LA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSAFISHWA ZAIDI.
Do you like this story?
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akitoa taarifa ya kikao cha
kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
|
Jumla
ya kata 22 katika manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke zitaingizwa
katika mpango wa utengaji wa maeneo maalum (smart area) kwa ajili ya
kuboresha usafi wa mazingira jijini Dar es salaam.
Akitoa
taarifa ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Dar es salaam (RCC) leo
jijini Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema
uanzishaji wa maeneo maalum ya usafi wa mazingira unalenga kuondoa shughuli
zote zinazofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji kinyume cha
sheria na kulifanya jiji la Dar es salaam kuendelea kuwa katika hali
isiyoridhisha ya usafi wa mazingira.
Amesema
utekelezaji wa mpango huo wa utengaji wa maeneo maalum unazingatia sheria ya
mipango miji Na. 8 ya mwaka 2007 na sheria ya mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 na
kuzitaja kata zitakazohusika katika mpango huo kuwa ni pamoja Keko,
Chang’ombe, Kurasini, Mibulani , Sandali na kata ya Gerezani zote za manispaa
ya Temeke.
Kata
nyingine ni Mchafukoge, Kariakoo, Mchikichini, Jangwani, Kisutu,
Kivukoni,Upanga Mashariki na Upanga Magharibi ambazo ziko manispaa ya Ilala na
kata za Hananasif, Kinondoni, Kigogo, Mzimuni na Magomeni zote za manispaa ya
Kinondoni.
Amesema
kuwa ili kufanikisha utekelezaji wa mpango huo hatua mbalimbali
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuondoa shughuli zote zinazosababisha kero
katika eneo husika, biashara zisizo rasmi, biashara za vyakula, uchomaji nyama
na mahindi kando kando ya barabara na maeneo ya watembea kwa miguu, uondoaji wa
gereji bubu, maguta, mikokoteni bajaji na bodaboda katikati ya jiji.
Shughuli
nyingine zitakazofanyika ni zile za uondoaji wa malori makubwa yenye zaidi ya
tani 10 katika maeneo yasiyoruhusiwa na kubainisha halmashauri zinaendelea
kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli hizo.
“Halmashauri
zetu zinaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli zote tulizoziainisha kwa
ajili ya shughuli mbalimbali za wananchi japo kuna maeneo tuliyoyatenga kwa
wananchi hayatumiki na baadhi ya wahusika hawako tayari kwenda kwenye maeneo
hayo” amesema.
Kuhusu
waendesha bodaboda na bajaji kuendelea kuingia katika maeneo yasiyoruhusiwa
hususani katikati ya jiji la Dar es salaam amesema kuwa serikali haitalifumbia
macho suala hilo kwa kuwa liko kisheria.
Amesema
watekelezaji wa sheria ya SUMATRA ya kuhifadhi maeneo yaliyotengwa wanaendelea
na zoezi la kuwaondoa wote wanaovunja sheria hiyo na kutoa wito kwa wahusika wa
zoezi hilo kuliendesha kwa kufuata sheria, taratibu na kuzingatia utu na haki
za binadamu.
“Nimeshatoa
maagizo kwa watendaji na viongozi wanaosimamia zoezi hili wahakikishe
wanaheshimu utu na haki za binadamu, kama ni kampuni ikigundulika tutaifungia
isipate tenda zozote za serikali, nachosema wahusika wawe makini serikali hatutawavumilia
wanaoendesha vitendo vya hujuma, uonevu, wizi, uporaji na ukiukaji wa haki za
binadamu” Amesisitiza.
Aidha
ameeleza kuwa mkoa wa Dar es salaa licha ya kukabiliwa na changamoto
ya ufinyu wa bajeti unaendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zenye
tija kwa maendeleo ya wananchi zikiwemo Elimu, Afya, ujenzi na ukarabati wa
barabara, madaraja na miundombinu mingine ya jiji ambayo imeharibiwa na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Amesema
katika kuimarisha huduma za afya mkoa kupitia kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)
imepitisha maombi maalum ya zaidi ya shilingi bilioni 45 nje ya bajeti ili
kukabiliana na tatizo la msongamano mkubwa wa wagonjwa wa nje na wale
wanaolazwa katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam.
Amesema
kuwa mkoa wake unapata wagonjwa wengi wa nje kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo
ya Kisarawe, Mkuranga, Mafia, wilaya ya Bagamoyo,Kibaha na Chalinze jambo
linaloongeza mzigo kwa hospitali za mkoa huo.
“Mkoa
wa wetu wa Dar es salaa una idadi kubwa ya watu kuliko mikoa mingine nchini pia
unahudumia watu wengine wengi kutoka maeneo mbalimbali, jambo hili linaongeza
mzigo kwa hospitali zetu kutokana na kuwahudumia wananchi kutoka nje ya mkoa”
Amesisitiza.
Ameeleza
kuwa wagonjwa wa nje sasa wanafikia 1500 hadi 2000 kwa siku jambo linalowafanya
kuomba fedha zaidi kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa hospitali za rufaa za
mkoa na ujenzi wa hospitali maalum kwa ajili ya mama na motto itakayokuwa na
uwezo wa kulaza wagonjwa 600 kwa wakati mmoja.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki ameeleza kuwa
mkoa wake una dhamira ya kuongeza maeneo mapya ya utawala kwa kuongeza kata 113
na mitaa 570 pamoja na kupitia mapendekezo yaliyowasilishwa kwenye kikao Maalum
cha kamati ya ushauri ya mkoa na mabaraza ya madiwani ya
halmashauri husika kuhusu kuugawa mkoa wa Dar es salaam katika
muundo wa wilaya 5.
Amesema
kuwa wilaya zilizopendekezwa ni pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, wilaya ya
Kigamboni na wilaya ya Ubungo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ JIJI LA DAR ES SALAAM KUENDELEA KUSAFISHWA ZAIDI.”
Post a Comment