Monday, April 28, 2014
MAADHIMISHO YA SIKU YA VYOMBO VYA HABARI KUFANYIKA ARUSHA.
Do you like this story?
WAANDISHI wa habari nchini wanatarajiwa
kuungana na wenzao duniani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya
Habari Duniani (WPFD), yanayotarajiwa kufanyika Mei 2-3.
Akitangaza sherehe hizo jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Jangwa la
Sahara (MISA), Mohammed Tibanyendera, alisema maadhimisho hayo
yatakayowashirikisha washiriki zaidi ya 200 yatafanyika jijini Arusha.
Alisema sababu za maadhimisho hayo
kufanyika Arusha ni kupata mrejesho wa maazimio waliyoyafikia kwa kuyapatia
kaulimbiu ya “Mount Meru Declaration”.
Alibainisha baadhi ya mambo
waliyokubaliana katika maadhimisho kama hayo mwaka jana yaliyozishirikisha nchi
jirani, ni pamoja na kuboresha hali za wanahabari.
Tibanyendera alisema katika sherehe
hizo kunatarajiwa kuzinduliwa machapisho mbalimbali, ikiwamo ripoti ya hali ya
vyombo vya habari Tanzania 2014.
Ripoti nyingine itakuwa utafiti wa
vyombo vya habari 2014 na ripoti ya uvunjifu wa uhuru wa vyombo vya habari kwa
mwaka 2014.
Alisema katika maadhimisho hayo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa aliyekuwa Jaji Mkuu na Mwanasheria, Mark Bomani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAADHIMISHO YA SIKU YA VYOMBO VYA HABARI KUFANYIKA ARUSHA.”
Post a Comment