Wednesday, April 2, 2014

MJUMBE ATAKA JK APEWE TUZO YA KATIBA.




Mjumbe wa Bunge la Katiba, Yusuph Manyanga amependekeza Bunge hilo na Serikali kuandaa tuzo maalumu ya kumpatia aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho.
Aliliambia gazeti hili kuwa pamoja na kuliendesha Bunge hilo bila kanuni, Kificho alilimudu na kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati ule.

Manyanga ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), alisema licha ya Kificho, pia tuzo apewe Rais Jakaya Kikwete kutokana na kuanzisha mchakato huo wa mabadiliko ya Katiba.

“Suala la kuandika Katiba katika mazingira ya amani siyo dogo, ni lazima tumpongeze Rais Kikwete kwa Tuzo ya Heshima, kwani ni busara zake tu ambazo zimewezesha jambo hili,” alisema Manyanga.

Kuhusu mchakato wa Katiba, alisema ni imani yake kuwa Katiba bora itapatikana, lakini akatoa wito wa wabunge na wawakilishi kutohodhi mijadala bungeni kwani hakuna aliye mzoefu katika Bunge la Katiba.

0 Responses to “MJUMBE ATAKA JK APEWE TUZO YA KATIBA.”

Post a Comment

More to Read