Wednesday, May 7, 2014
KOCHA MBEYA CITY FC: `YOUNG FUTURE TAIFA STARS` YA POULSEN NDIO INGEWEKWA KAMBINI TUKUYU NA SI VIJANA HAWA WA MABORESHO
Do you like this story?
MCHAKATO wa maboresho ya timu ya taifa
ya Tanzania, Taifa stars uliohusisha makocha mbalimbali kuzunguka mikoani kwa
lengo la kung`amua vipaji vilivyofichika
umeendelea kukosolewa na baadhi ya wataalamu wa soka.
Akizungumza na mtandao huu, kocha
msaidizi wa Mbeya City fc, Maka
Mwalwisyi amesikitishwa sana na shirikisho la soka Tanzania TFF, kuamua kutumia
mfumo huu badala ya kuhangaika kujenga msingi wa soka ambao ndio kilio cha
watanzania wengi.
Maka alisema watanzania kwasasa
hawahitaji kuona TFF inahangaika na timu ya Taifa kwa kutafuta wachezaji
wasiocheza ligi kuu, kwasababu kupata mafanikio kwa mfumo wa sasa ni ngumu sana
na hata mataifa makubwa hayawezi kutengeneza timu ya taifa inayojiandaa na
mashindanio mwaka mmoja mbele kwa mfumo huu.
“Mimi nashangaa sana na nitaendelea
kushangaa, kwanini makocha walipitisha mpango huu?, hivi kama kweli mchezaji
yupo Mbeya na ana kiwango cha juu, sisi Mbeya City tutashindwa kumuona kweli?
Hata wenzetu Prisons wasimuone, hapana”.
‘Wanachagua makocha kuzunguka nchi
nzima na kutumia fedha nyingi, sidhani kama ni suluhisho, kuna mambo mengi ya
kuyafanya hasa kujenga misingi ya soka la vijana”.
“Mchezajai hachezi ligi, unamchukua
kutoka mchangani na kumleta Taifa stars, halafu unawadanganya watanzania kuwa
unataka uipeleke timu AFCON mwakani nchini Morocco”.
‘Hivi huyu mchezaji ambaye hachezi
ligi, itakuwaje akikutana na wachezaji wanaoshindia mpira kama magharibi mwa
Afrika?, hivi ni vichekesho tu”. Alisema Maka.
Kocha huyo aliongeza kuwa TFF
wangeshauriwa kuendeleza timu ya `Young Future Taifa stars` iliyoanzishwa na
kocha aliyevunjiwa mkataba, Mdenish Kim Poulsen kwasababu ilijumuisha wachezaji
wa ligi kuu.
“Kim alikuja na mpango mzuri, lakini
wameona kama haufai”.
“ Ile timu ya Young Future Taifa stars
ndio ingewekwa kambini miezi miwili Tukuyu, angalau tungepata watu fulani”
“ Lakini kwa kikosi chao kile cha
maboresho, hawajafanya kitu pale na nashukuru watanzania kugundua hilo
kwasababu nawasikia wakisema”.
“Nadhani kocha Mart Nooij aliwaambia
kuhusu wachezaji hawa. Niliwaona na kugundua kuwa hawana msaada kwa Stars. Ndio
maana hawakupangwa hata kwenye mechi dhidi ya Malawi”.
“Rais Malinzi na watu wake wakae chini
tena kuufikiria mfumo huu. Nadhani si busara kuacha kila lililokuwa linafanywa
na watu wa nyuma”.
“Mazuri yaendelezwe na mabaya
yasahihishwe , lakini kwa mwendo huu nakuw a na mashaka”.
‘Unashindwa kuchukua wachezaji kutoka
Mbeya City fc iliyomaliza nafasi ya tatu”
“ Unakwenda kutafuta watu wasiojulikana
kwa kutumia fedha nyingi na hawachezi ligi, hakika unaleta utani tu”. Alimaliza
Maka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOCHA MBEYA CITY FC: `YOUNG FUTURE TAIFA STARS` YA POULSEN NDIO INGEWEKWA KAMBINI TUKUYU NA SI VIJANA HAWA WA MABORESHO”
Post a Comment