Friday, May 9, 2014

MAHAKAMA KUU YAMFUTIA KESI PROFESA COSTA MAHALU.




MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,HIvi PUNDE imemfutia rufaa ya Kesi ya uhujumu uchumi Na.1/2007 iliyokuwa ikimkabili Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Ricky Mahalu na Grace Martin Waliokuwa wakitetewa na Mawakili wa kujitegemea Beatis Malima, Mgongolwa,Cuthbert Tenga na Mabere Marando , iliyokuwa imekatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), dhidi ya Mahalu na Grace Kapinga hukumu ya iliyotolewa na Aliyekuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ya Agosti 9 Mwaka 2012,Elvin Mugeta ambayo hukumu hiyo iliwaachiria Huru wa jibu rufaa ambao walikuwa wakikabiliwa na Kesi ya uhujumu Uchumi wa zaidi Ya Euro Milioni mbili Katika ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.

Jaji John Utamwa Alifikwa uamuzi wa kutoa amri ya Kuiondoa RUFAA hiyo iliyokuwa imekatwa na DPP dhidi ya Mahalu na Grace kufuatia ombi lililowasilishwa na DPP Mwenyewe lililokuwa likiomba Mahakama hiyo iondoe RUFAA hiyo aliyokuwa ameikata dhidi ya wa jibu RUFAA hicho chini ya Kifungu Cha 386(1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Mwaka 2002 kwasababu DPP Hana Haja ya kuendelea na rufaa hiyo.

0 Responses to “MAHAKAMA KUU YAMFUTIA KESI PROFESA COSTA MAHALU.”

Post a Comment

More to Read