Friday, May 23, 2014
MALERIA; MATUMAINI YA KUPATIKANA KINGA.
Do you like this story?
Watafiti
wa Marekani wamebaini miili ya watoto hao hutoa viini vya kinga ambavyo
hushambulia wadudu wanaosababisha Malaria.
Kwa
kumdunga mtu sindano yenye viini hivyo vyo mtu anaweza kukingwa na ugonjwa huo
.
Watafiti
hao ambao walichapisha matokeo yao kwenye jarida la kisayansi , wanasema
majaribio ya utafiti huo katika binadamu na katika sokwe sasa yanahitaji
kutathminiwa kikamilifu ili kupata matumaini halisi ya chanjo ya malaria.
Prof
Jake Kurtis, mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa afya wa kimataifa katika
hospitali ya kisiwa cha Rhode katika chuo kikuu cha tiba cha Brown , alisema :
"Nadhani kuna ushahidi wa kuaminika kwamba hii inaashiria upattikanaji wa
chanjo ''
"
Hata hivyo wadudu wa malaria ni vigumu kuwashambulia'' . Kwa kweli ni maadui
wakubwa ." aliongeza Kurtis. Utafiti huo ulianza kwa kundi la watoto wa
shule 1000 nchini Tanzania , ambao sampuli za damu yao zilichunguzwa mara kwa
mara katika miaka ya mwanzo ya maisha yao .
Asilimia
6 ya watoto ya watoto hawa waliweza kuwa na kinga asilia kwa malaria, licha ya
kuishi katika eneo ambako ugonjwa huo umekithiri.
Chanzo:Bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MALERIA; MATUMAINI YA KUPATIKANA KINGA.”
Post a Comment