Tuesday, May 6, 2014

MUUMIN AZIKOSOA TUZO TATU ZA MUZIKI WA DANSI ZILIZOTOLEWA KWA JOSE MARA, FERGUSON NA MASHUJAA BAND




MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi, Mwinjuma Muumin amezikosoa tuzo tatu za muziki wa dansi zilizotolewa Jumamosi, Mlimani City katika usiku wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

 Muumin alitoa tathmini yake jana mchana ambapo amesema hakubaliani na Mashujaa Band kupewa tuzo ya bendi bora ya mwaka, hakubaliani pia na Jose Mara kuwa mwimbaji bora wa mwaka huku pia akishangaa Ferguson kuwa rapa bora wa mwaka.

Mwimbaji huyo ameshangaa bendi kama FM Academia au Twanga Pepeta kukosa tuzo ya bendi bora, lakini akashangaa zaidi Jose Mara anakuwaje mwimbaji bora mbele ya mtu kama Christian Bella halafu Ferguson ampiku Totoo ze Bingwa au Kitokololo.  

0 Responses to “MUUMIN AZIKOSOA TUZO TATU ZA MUZIKI WA DANSI ZILIZOTOLEWA KWA JOSE MARA, FERGUSON NA MASHUJAA BAND”

Post a Comment

More to Read